Dalili 7 kuwa mpenzi wako anakusaliti.

DJ SEPETU

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
8,413
12,328
Migogoro ni sehemu ya maisha Na wengine huita ndio mapenzi yenyewe Na unaweza vumilika.

Usaliti ni suala linaloumiza Na kukatisha tamaa sana.kama kuna mabadiliko unayashuhudia kwa mtu wako Na bado hujafahamu sababu,pindi uonapo ishara hizi inabidi kumtolea uvivu Na kumfungukia mchana kweupe!,kwani sio ajabu Mali zako zinaliwa Na wajanja.

7.kujiremba kumezidi.
Ni jambo zuri kwa mtu kuwa Mrembo Na mtanashati,ila kukiona imekuwa zaidi ya kawaida yake maana yake ni kua anajaribu kumridhisha mtu Fulani mbali Na wewe,kazini,kanisani au chuoni.

6.hataki uguse simu yake.
Kila mtu anahitaji faragha,ikiwa ukishika simu yake anawaka,au neno siri limebadilishwa ghafla,atakuwa anawasiliana Na mtu Na hataki ujue.

5.anapunguza hamu ya tendo
Kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ktk uhusiano,ikiwa visababu vinakuwa vingi sana INA maana hajisikii kufanya mapenzi Na wewe.

4.rafiki zimwi
Wanaume Na wanawake huwa Na marafiki Wa jinsia nyingine,kama kuna rafiki ambaye ukaribu wao umepindukia, amka!

3.anakufananisha Na wengine
Hii ni dalili Kali sana kuonyesha mzigo huo unaliwa!kufoka foka kwa mambo madogo,kuna mwingine anayeonyeshwa mapenzi ya dhati kuliko wewe!

2.Anakutenga.
Anapunguza mawasiliano nawe,pia anawahepa marafiki zako.

1.Anageuza neno tu kuwa ni
Tu huwa kitu kimoja kwa wapenzi,sasa ukiona anarudi kutumia ni maana yake ni kwa anakufuta taratibu maishani mwake.

Bonasi ni kuwa ukiona mapenzi yamezidi kuliko kawaida mfano zawadi kibao INA maana dhamira yake inamsuta sasa anapunguza maumivu ya kukusaliti moyoni mwake kwa kuuma Na kupuliza .

Pia nyakati zingine anaweza kukataa kufanya mapenzi sababu ya maradhi au msongo Wa mawazo.

Jichunguze pia wewe mwenyewe unaweza kuwa chanzo cha yeye kukusaliti.
 
Unashangaa mtu yuko bize kumchunguza mpenzi wake kama anamsaliti wakati yeye mwenyewe ni msariti. Sasa hui muda unaotumia kumchunguza mwenzako kwa nini usiutumie kujirekebisha tabia yako, Newton alisema " action and reaction are equal but in opposite direction" kwa hiyo ukiwa msaliti utasilitiwa tu. Mapenzi ni kuaminiana tu inatosha si kuanza kufuatana fuatana. Tena ukijifanya mkuda utapigiwa machoni mwako huku unaona. Kama humuamini mpenzi wako kwa nini unakaa nae, si umwache tu..
 
Back
Top Bottom