Naam mpenzi msikilizaji, ni dakika ya 44 ya mchezo nusu fainali kati ya KAMATI YA UCHAGUZI v/s CCM, KOMBE LA URAIS, mpaka sasa hakuna timu iliyokwisha ona lango la mwenzie, haya sasa anakwenda kule Malechela, vizuri kabisa anamtangulizia Nape, anakwenda Nape, Nape, Nape hatari kuleee nini?
Faulo!, na unatokea mzozo pale, RED CARD zinatembea, ndugu msikilizaji Red Card Zinatembea, wachezaji takribani 6 wa CCM wanapewa kadi nyekundu kwa utovu wa nidhamu akiwemo foward wao Edward Lowassa_Maradona, analalama huku Sumaye,
CCM watacheza wakiwa watano uwanjani, na kama watashinda leo watapambana na timu ya UKAWA kwenye hatua ya fainali itakayochezwa October Mwaka Huu pale uwanja wa Bungeni Mjini DODOMA, sasa kama foward wao tegemezi ndo hivo amepewa RED CARD inamana ataikosa mechi hiyo na sidhani kama watashinda.
Haya anaenda kucheza faulo ile Jah_kaya, anacheza kwake Nape, naam mpira ni mapumziko, dkk 45 za kipindi cha kwanza zinakatika.
Wakati tukiwa mapumziko, hebu tupate maoni mawili matatu kutoka kwa wadau.