Dagaa Nyasa wanauzwaje huko kwenu?

Sijawahi kuwala hawa dagaa.ebu nielezee utamu wake niwatafute...
 
sumbawanga wanauzwa tzs 12,000 kwa kilo. ila mbona wabaya kwangu! kwanza huwezi kuelewa kama ni dagaa au samaki. pili ni wagumu kuiva. binafsi siwapendi
 
sumbawanga wanauzwa tzs 12,000 kwa kilo. ila mbona wabaya kwangu! kwanza huwezi kuelewa kama ni dagaa au samaki. pili ni wagumu kuiva. binafsi siwapendi

Hawa wanafaa zaudi wakiwa wabichi.....
 
sumbawanga wanauzwa tzs 12,000 kwa kilo. ila mbona wabaya kwangu! kwanza huwezi kuelewa kama ni dagaa au samaki. pili ni wagumu kuiva. binafsi siwapendi

Hawa Dagaa kama huwezi kuwapika utawachukia sana lakini ukiweza kuwapika maisha ni murua hawapikwi kama dagaa wengine wenyeji wa mkoa wa Ruvuma wanalijua hilo, lazima uwaloweke na walowane sana kama umechelewa kuwaloweka wachemshe hadi walinike, (na ukiwa unawaloweka weka na chumvi kabisa) weka tui la karanga au Nazi halafu kula na wali, huku songea sado (sawa na kilo 4) shs 5,000/=
 
Kudadeki inawezekana sijapata wa kuwapika ipasavyo...ukila wako kama unatafuna mbao...
 
true songea sado 5000 ila hufika hadi 8000. tume pesa utumiwe mzigo superfeo
 
Hivi kisado kile wanafika kg 4? Mbona ni kama mgodi utembeao hivi kwani dar n ni 10000 per kg!!
 
true songea sado 5000 ila hufika hadi 8000. tume pesa utumiwe mzigo superfeo

Mi nipo songea!! Nataka kutoka huku na kuuza sehemu nyingine kama dar hivi!!

So am doing market research!!
 
jamani sunbawanga ni balaa kwa bei ya hao dagaa. nilimwagiza dada wa kusaidia kazi akaniambia elf 12 kwa kilo(hawauzi kwa sado huku). sikumwamini sana ila nikamezea tu. shughuli ilikuja wakati wamepikwa. kama mbao kwa kwelo. ukweli sikuweza kuwala. hapa pia kuna dagaa wa ziwa tanganyika. wenyewe ni tzs 4000/kg. wenyewe ni wazuri na wadogo. wa victoria wapo ila si wazuri kwa sababu ya handling. unajua dagaa wa victoria are so delicate. wanahitaji umakini kuwatunza. hivyo kuna soko hapa la dagaa wa nyasa
 
Kuna dagaa aina mbili ziwa Nyasa. Wa Kyela ni wadogo na laini sana, pia ni watani mno. Wanaiva haraka sana. Wa songea ni wakubwa sana na wagumu sana na ndiyo wanapatikana sehemu nyingi hapa nchini. Wa Kyela wanapatikana huko huko tu
 
ok. kwanin kyela vizuri mnskula wenyewe? anyway nitamwambia rafiki yangu ulimboka aniletee hao wa kyela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…