Dada zangu, maisha baada ya kustaafu yatakuwaje?

Keneth12

Senior Member
Oct 12, 2015
114
162
Wana Jf
Naomba niseme kwamba kuna maisha baada ya kustaafu kazi anayoifanya mdada au anavyojibidiisha ndio itakayo msaidia pindi atakuwa hana nguvu ya kutafuta hapa sitawazungumzia wanaume; dada zetu wengi nawagawanya katika makundi na kila kila kundi kijitathmini kwa kuangalia umri na amejipanga vipi baada ya kustaafu kazi anayoifanya au anajipangaje ili aweze kuendelea kuishi baada tu ya kufikia umri ambao mwili hauwezi tena kutafuta kwa kasi na nguvu kubwa.

Kundi 1: Kina dada wafanya kazi secta isiyo rasmi, lazima wajipange wasijisahau, wasiishie kuvaa nguo za thamani na kupenda vitu vya thamani bila ya kuandaa mazingira ya kustaafu, lolote laweza likatokea katika maisha na huenda ndio itakuwa mwisho wako wakutafuta aukupata rizki sasa utafanyaje, kujipanga lazima iwe juhudi za kila siku ikiwemo kuweka akiba ambayo hutaweza kuifikia na kuitumia, akiba hiyo iwe ya malengo ya badae hata kama itakuwa kidogo kiasi gani ilimradi uwe unamaanisha. Fanya wewe kama wewe usimtegemee mtu mwingine hata mume usimtegemee sana simama wewe kama wewe.

Kundi 2: Wanaofanya kazi katika sekta zilizo rasmi, pamoja na uhakika wa mshahara hata uwe mdogo kiasi gani jifunze kujinyima ila baada ya miaka kadhaa nawewe uwe mtu flani, mikopo tunayoichukua ni ya kukuwezesha kwa haraka ufanye kitu flani ila bado kiwango hicho unacho katwa unaweza ukaamua kukiweka kila mwezi ukizidisha kwa muda ambao ungechukulia mkopo na hivyo kufanya kitu cha maana kuliko kuchukua mkopo na kuendelea kuishi na stress.

Kundi 3: Wanaotafuta waolewe na wanaume wenye pesa na uwezo wa kifedha kwanini tusijitume wenyewe kutafuta kuliko kusubiri wanaume wa aina hiyo? Kwanini tusiungane na hao tunao olewa nao na tuanze kutafuta wote na wale tunao olewa nao, kuna mateso flani ambayo huwa yapo kwa kumtafuta mwanaume aliye nacho na kuna mateso flani kwakuwa ulimtafuta aliye nacho hivyo kuteseka maana mapenzi ya dhati hayakiwepo, jibidiishe na umtafute mwenye mapenzi mema na ambaye ni chaguo la mwenyezi Mungu huyu atakusaidia katika kupangilia maisha na kujibidiisha hadi kufikia umri wa kustaafu muwe mmeshajiandaa unaweza hata usiyafikie malengo yako kwa kutafuta kuolewa na mtu mwenye maisha mazuri au tajiri kweli huwa inatokea kwa wengi maana walipenda kwa tamaa.

Kundi 4: Kinadada wasio na kazi, tuache vijitabia ambavyo vitakuwa kikwazo mbele ya safari, leo hii unaweza usione madhara yake ila umri utakapokuwa umeenda ndio utaona, kujiheshimu ni swala la msingi, kujithamini, kujitambua na kutokuwa mjanja mjanja ni jambo jema sana katika maisha, tulia omba Mungu akupe rizki, akupe chema, akupe wepesi katika maswala yote unayoyafanya, fanya kitu kwa malengo usikubali kudanganywa na zaidi sana usizae hovyo bila ya kuwa na mwanaume wa uhakika na mwenye malengo, wanaume wengi wana tamaa na kuwandanganya wasichana kama huna mpango na yeye kaone nyota ya kijani ili uwe salama.

Kundi 5: Wanaopata pesa za msimu, lazima tujipange, kuringishiana kuvaa au kuwa na vitu vya thamani kutatuaibisha mbele ya safari, weka akiba na hazina unapopata jitahidi kuishi maisha ya kawaida na kuwekeza zaidi katika miradi ya uzalishaji na ya kudumu na iwe chanzo cha kuanzisha miradi yote usifanye mchezo maana uta ahibika.

Kina dada wengi wanateseka sasa hivi, waliwahi kupata fedha na kuwa maarufu leo hii wamehama mikoa na kujikuta wameambulia maradhi ambayo hayatibiki, lazima tujipange kwa badae, waliokuwa wajanja wamestaafu na sasa hivi wapo maeneo walipochukua mashamba na kuwa wakulima na hivyo kuendelea kuwa na kipato huku wakifurahia kazi za mikono yao pindi walikuwa bado wana nguvu.

Swala lingine kwa makundi yote ni kuhusu harusi kwa watakao bahatika unapompata mwenza wa maisha uliyepewa na mwenyezi Mungu jaribu kuangalia uwezo alio nao na kupanga baada ya harusi mtafanya nini, kuna kama kuwekeza na kuanzisha mradi flani miezi michache au mwaka au miwili baada ya harusi sio kukaa tu hapana maana kuna siku na isiyosiku.

Kwa kinadada wengine kabla ya kumkubalia mchumba wako kufanya harusi yenye thamani kubwa kwanza tathmini uwezo wake wa kifedha kwanza maana harusi zina gharama kubwa sana, wengi wamefunga na kubaki na madeni sasa mdada panga kama vile ingekuwa ww ndio umetoa iyo pesa na unapangilia kuwa utakaa ndani ya miezi 6 hadi mwaka hutajuwa na tatizo la chakula na mahitaji ya muhimu ndani kwako, bado mdada una uwezo wa kutoa taarifa kwenu kuwa iyo pesa ya harusi itusaidie kuanzisha mradi wa uzalishaji ila mtaenda msikitini, kanisani, serikalini au kwenye mila kwa utaratibu wa kawaida kwa gharama ndogo sana au mtaenda na washenga tu mkayamalize mialiko ya watu wengi kuja kula na kunywa mnaipotezea, hao hao mnaowaalika kuja kula na kunywa kwa sherehe za mbwembwe ndio watakuwa wakwanza kuwacheka mtakapokuwa mnadaiwa na kukosa chakula ndani sasa lazima tulitazame hili tusije tukaaibika mbele ya safari.
 
Haya maneno yanakaribiana na maneno niliyowapa jana rafiki zangu, niliwaambia hivi inakuwaje una cm ya laki mbili mkononi halafu unalalamika ajira hakuna na maisha uliyojizoesha ya matawi ya juu kiasi kwamba huwezi kufanya biashara ndogo ndogo, umri unaenda umeshindwa kutumia cm ya elfu sabini change inayobaki uanzishie mradi? Jibu lake eti nilihongwa hiyo cm, biashara ya mandazi mtaji haufiki laki moja napo umeshindwa hata anayekuhonga naye zuzu tu, ukuanza kidogokidogo utajifunza kuwa na kikubwa ndo utajifunza na kuweka akiba ya badaye siyo ukipata elfu hamsini kesho hata kumi huna, mume akikupa hela ya matumizi unatumia yote hata akiba huna
 
Kama unahitaji kitabu nlichokiandika kimeandikwa HOFU YA NINI kinatoa mifano ya watu waliotumia pesa vizuri na vibaya na kujaribu kutoa mwanga kwa wanaotaka kuweka akiba jinsi ya kugawana mapato ya kila siku. Kina patikana soft copy na hard copy wasiliana na 0767353513
 
Wana Jf
Naomba niseme kwamba kuna maisha baada ya kustaafu kazi anayoifanya mdada au anavyojibidiisha ndio itakayo msaidia pindi atakuwa hana nguvu ya kutafuta hapa sitawazungumzia wanaume; dada zetu wengi nawagawanya katika makundi na kila kila kundi kijitathmini kwa kuangalia umri na amejipanga vipi baada ya kustaafu kazi anayoifanya au anajipangaje ili aweze kuendelea kuishi baada tu ya kufikia umri ambao mwili hauwezi tena kutafuta kwa kasi na nguvu kubwa.

Kundi 1: Kina dada wafanya kazi secta isiyo rasmi, lazima wajipange wasijisahau, wasiishie kuvaa nguo za thamani na kupenda vitu vya thamani bila ya kuandaa mazingira ya kustaafu, lolote laweza likatokea katika maisha na huenda ndio itakuwa mwisho wako wakutafuta aukupata rizki sasa utafanyaje, kujipanga lazima iwe juhudi za kila siku ikiwemo kuweka akiba ambayo hutaweza kuifikia na kuitumia, akiba hiyo iwe ya malengo ya badae hata kama itakuwa kidogo kiasi gani ilimradi uwe unamaanisha. Fanya wewe kama wewe usimtegemee mtu mwingine hata mume usimtegemee sana simama wewe kama wewe.

Kundi 2: Wanaofanya kazi katika sekta zilizo rasmi, pamoja na uhakika wa mshahara hata uwe mdogo kiasi gani jifunze kujinyima ila baada ya miaka kadhaa nawewe uwe mtu flani, mikopo tunayoichukua ni ya kukuwezesha kwa haraka ufanye kitu flani ila bado kiwango hicho unacho katwa unaweza ukaamua kukiweka kila mwezi ukizidisha kwa muda ambao ungechukulia mkopo na hivyo kufanya kitu cha maana kuliko kuchukua mkopo na kuendelea kuishi na stress.

Kundi 3: Wanaotafuta waolewe na wanaume wenye pesa na uwezo wa kifedha kwanini tusijitume wenyewe kutafuta kuliko kusubiri wanaume wa aina hiyo? Kwanini tusiungane na hao tunao olewa nao na tuanze kutafuta wote na wale tunao olewa nao, kuna mateso flani ambayo huwa yapo kwa kumtafuta mwanaume aliye nacho na kuna mateso flani kwakuwa ulimtafuta aliye nacho hivyo kuteseka maana mapenzi ya dhati hayakiwepo, jibidiishe na umtafute mwenye mapenzi mema na ambaye ni chaguo la mwenyezi Mungu huyu atakusaidia katika kupangilia maisha na kujibidiisha hadi kufikia umri wa kustaafu muwe mmeshajiandaa unaweza hata usiyafikie malengo yako kwa kutafuta kuolewa na mtu mwenye maisha mazuri au tajiri kweli huwa inatokea kwa wengi maana walipenda kwa tamaa.

Kundi 4: Kinadada wasio na kazi, tuache vijitabia ambavyo vitakuwa kikwazo mbele ya safari, leo hii unaweza usione madhara yake ila umri utakapokuwa umeenda ndio utaona, kujiheshimu ni swala la msingi, kujithamini, kujitambua na kutokuwa mjanja mjanja ni jambo jema sana katika maisha, tulia omba Mungu akupe rizki, akupe chema, akupe wepesi katika maswala yote unayoyafanya, fanya kitu kwa malengo usikubali kudanganywa na zaidi sana usizae hovyo bila ya kuwa na mwanaume wa uhakika na mwenye malengo, wanaume wengi wana tamaa na kuwandanganya wasichana kama huna mpango na yeye kaone nyota ya kijani ili uwe salama.

Kundi 5: Wanaopata pesa za msimu, lazima tujipange, kuringishiana kuvaa au kuwa na vitu vya thamani kutatuaibisha mbele ya safari, weka akiba na hazina unapopata jitahidi kuishi maisha ya kawaida na kuwekeza zaidi katika miradi ya uzalishaji na ya kudumu na iwe chanzo cha kuanzisha miradi yote usifanye mchezo maana uta ahibika.

Kina dada wengi wanateseka sasa hivi, waliwahi kupata fedha na kuwa maarufu leo hii wamehama mikoa na kujikuta wameambulia maradhi ambayo hayatibiki, lazima tujipange kwa badae, waliokuwa wajanja wamestaafu na sasa hivi wapo maeneo walipochukua mashamba na kuwa wakulima na hivyo kuendelea kuwa na kipato huku wakifurahia kazi za mikono yao pindi walikuwa bado wana nguvu.

Swala lingine kwa makundi yote ni kuhusu harusi kwa watakao bahatika unapompata mwenza wa maisha uliyepewa na mwenyezi Mungu jaribu kuangalia uwezo alio nao na kupanga baada ya harusi mtafanya nini, kuna kama kuwekeza na kuanzisha mradi flani miezi michache au mwaka au miwili baada ya harusi sio kukaa tu hapana maana kuna siku na isiyosiku.

Kwa kinadada wengine kabla ya kumkubalia mchumba wako kufanya harusi yenye thamani kubwa kwanza tathmini uwezo wake wa kifedha kwanza maana harusi zina gharama kubwa sana, wengi wamefunga na kubaki na madeni sasa mdada panga kama vile ingekuwa ww ndio umetoa iyo pesa na unapangilia kuwa utakaa ndani ya miezi 6 hadi mwaka hutajuwa na tatizo la chakula na mahitaji ya muhimu ndani kwako, bado mdada una uwezo wa kutoa taarifa kwenu kuwa iyo pesa ya harusi itusaidie kuanzisha mradi wa uzalishaji ila mtaenda msikitini, kanisani, serikalini au kwenye mila kwa utaratibu wa kawaida kwa gharama ndogo sana au mtaenda na washenga tu mkayamalize mialiko ya watu wengi kuja kula na kunywa mnaipotezea, hao hao mnaowaalika kuja kula na kunywa kwa sherehe za mbwembwe ndio watakuwa wakwanza kuwacheka mtakapokuwa mnadaiwa na kukosa chakula ndani sasa lazima tulitazame hili tusije tukaaibika mbele ya safari.

Asante mkuu..kama msichana sikuwa navyo vyote nakushukuru sana aise kwa kuniongezea.ubarikiwe mku
 
Mimi naamini kama unafanya kazi kwa bidii na kutumiaulicho nacho vizuri hukuukimshirikisha Mungu kwa kila jambo.Hata ukikosa hicho ulochonacho utatoboa tu sehemu nyingine.Umetoa ushauri mzuri sana siokwa dada zetu tu ila ni kwa wote
 
Back
Top Bottom