Kuolewa ni rahisi sana endapo utakuwa mjanja unajitambua na unajua unachokifanya,
Wanaume tunapenda kuheshimiwa na kuona mwanamke anatii kile tulicho muambia afanye, wanaume tunapenda mwanamke anayeweza kuvumilia nyakati zote za shida na raha (pesa na msoto). ukiwa hauna hivi vigezo jaribu hata kuigiza kwa yule unayemtaka akuoe,
Nakuona barabarani nakusimamisha nakuomba namba unanipa usiku nakutongoza unankubalia hapo hapo unaniomba pesa ( nakudharau) kwa vile nshakujua nakupa unaniomba tena nakupa unajua hapa umepata kumbe umepatikana unakuja kwangu nakutafuna ukiondoka nakublock
mchakato unaanza tena mpaka nije nikutane na mwenye vigezo vilivyopo hapo juu, huyu sitaangalia kama ni mzuri kisura shepu nzuri n.k akiwa navyo vyote basi mungu kaleta. huyu ndiye atakaye kuwa malkia wangu ndiye atakaye chukua taji la ushindi kwa vile ameushinda mchujo.
Hiyo ndio principle yetu, mkishindwa kabisa jaribuni hata kufake life jifanyeni hampendi pesa kwa wale mnao watargert wawaoe hata kama mmewaona wana pesa nyingi.
mwanaume hata awe milionea anapenda mwanamke mwenye nidhamu ya pesa, ukiuruka huu mtego hata kuchezea atakuheshimu atakuonea huruma atakupa pesa hata kama huja muomba, atakushirikisha kwenye miradi yake.
Hio ndio limbwata ya kumnasa mwanaume aliyeshindikana kuoa.
Tafakari chukua hatua!