Dada wa kuuza mgahawani anahitajika

Dada wa kuuza mgahawani anahitajika

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,788
Reaction score
3,062
Habari.

Natafuta dada wa kuuza mgahawani.
Awe na sifa zifuatazo
1/Awe na miaka isiyopungua 15 na isizidi 20
2/Awe mchapakazi haswa, Aweze kufanya kazi kwa muda mrefu, kuanzia saa 12 asubuhi hadi sa 5 usiku kama wateja watakwepo
3/Awe na nidhamu ya hali ya juu, napenda zaidi mtumishi wa Mungu ili twende sawa. Mimi sipendi mhuni.
4/Awe msafi na mgahawa uwe safi muda wote.
5/Awe na lugha nzuri ya ushawishi, uhudumu pamoja na yote yale ya kuwavutia wateja karibu zaidi
6/Ajue kupika vyakula vitamu na vyenye ladha ya kimataifa.

-Muda wa kazi ni ni siku zote za kazi ila wikendi atapumzika ili afanye mambo yake binafsi.
-Aje na picha 4 za paspoti na barua ya mwakilishi wa nyumba 10 na mtendaji wa kijiji/mtaa anaoishi.
-Eneo la kazi ni maeneo ya chuo.
-Chumba cha kulala kipo na mahitaji yote muhimu ya binadamu yapo.
-Mshahara tutaongea.
-Mgahawa ni mkubwa kiasi.

NB: Vigezo na masharti kuzingatiwa! Iwapo unavigezo ni pm.
 
Huyo lazima awe kicheche wa tatu.........
 
Mfanyakazi mwenye sifa hizo unatakiwa usimlipe chini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kwa mwezi.
Umkatie na bima ya afya.
Na NSSF.
Halafu katikati ya mwezi uwe unampa posho.
Kula na kulala ni juu yako mwajiri.
Halafu umshonee na sare za kazini.
 
Sifa zote ninazo ila umri umesogea kidogo nipo songea kama hutajali ni pm.
 
Eneo la chuo??chuo kipi??mkoa/wilaya?vyuo vipo vingi mkuu..but i guess u mean chuo kikuu udsm?
 
Kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa5 usiku? Kawa sh ngapi?wabongo tunaumizana sana
 
Hapo utakuta ata unamlipa chin ya elf 10 alfu kuanzia 12 morning to 5 night kali duuh dhambi wewe
 
Heading: Dada wa kuuza mgahawani
Content: ajue kupika vyakula vyote
Age required: <15>20

Najiuliza kwa huo umri unaohitaji kama atakua na huo uwezo wa kufanya shughuli zote hizo mlipe kamilioni itapendeza zaidi.
 
Kwa umri hyo,na vgezo ulvyo weka mbona km haviendan,MF: elimu, ujuzi na uzoefu kwa umri huo c rahci.labda awe 25+
 
Yaani huyo huyo auze mgahawa na pia apike na kwa umri huo ina maana ni binti ambaye ndio kwanza amemaliza form four huo uzoefu na ujuzi wa kupika vyakula vyenye hadhi ya kimataifa ameupata wapi?
 
Kama ukimpata hakikisha anapata haki zake zote wala usimkandamize

Saa 12 hadi saa 5 usiku duuuuh! kumbuka hata na yeye ni binadamu. Kazi zinapoisha hiyo saa 5, kwa mahesabu ya haraka mpaka na yeye alale ni kama saa 6 hivi. Na kuamka hiyo saa 12 asubuhi, itamlazimu aamke saa 11 alfajiri kwa ajili ya kujiandaa. Kwahiyo anakuwa amelala masaa matano huku akiwa amefanya kazi masaa 17
Hapo kuna uonevu mkubwa sana
 
Screenshot_2018-02-16-20-21-43.png
ok
 
Back
Top Bottom