Dada wa kazi akimweleza mume wangu siri hii, sina ndoa tena

faith marie

Member
Feb 9, 2016
47
28
Mwaka jana mwishoni hubby na watoto walienda likizo kijijini kama utaratibu wa kila mwaka, nyumbani tukabaki mimi na msichana wa kazi, sikupewa likizo kazini, siku moja msichana wa kazi alinifuma na rafiki hapo nyumbani kwetu red handed na amelitumia suala hilo kama silaha dhidi yangu.

Kila Sunday huwa nampa ruhusa kwenda kanisani na nyumbani kusalimia, kwao ni hapa hapa mjini, huwa anaondoka asubuhi na kurudi jioni ya sa 6, hivyo rafiki yangu alinipigia simu kwamba tuonane hata kwa maongezi tu briefly, kwa kujua nipo alone home na kwamba ni maongezi mafupi nikamuomba rafiki aje nyumbani, kinyume na matarajio yetu tukashindwa kujizuia na kuanza romance ukumbini na baadae tukahamia bedroom kwa msichana wa kazi, niliona si vyema kutumia bedroom yangu.

Sijawahi kuelewa hadi leo kwanini huyu binti alirudi saa tisa badala ya jioni kama siku zote, ndani mwetu wote tulishagawana copy za funguo za geti dogo, hubby, mimi na hg, hivyo tukashtuka tu msichana wa kazi anafungua mlango na kuingia hivyo kutukuta kama tulivyozaliwa katikati ya suala lile.

Nilimgombeza sana kwa ukosefu wa adabu, maana badala ya kutoka nje akabaki humo anakodoa macho, then akatoka nje, nikajifunga khanga nikamfuata nikamuuliza kulikoni umerudi saa tisa? Hakujibu, hatukuongea kitu hadi kesho yake wakati naondoka kwenda kazini, nikaanza kumkaripia upya kuwa nisikie kasema chochote kwa mtu yeyote, cha kushangaza binti akaenda room na kurudi na begi lake kwamba anaondoka na atampigia simu daddy kumueleza alichoona, na hapo kanishikia kiuno, ikabidi nijishushe nimpigie magoti, nikambeleza sana na kumpa laki moja, akakubali kubaki.

Tangu hapo amekua mwiba mkali kwangu, mara leo aseme anataka smartphone namletea, kesho anataka laki, next day, laki mbili, vyote hivyo natoa kwa kuogopa kuvunja ndoa yangu, lakini zaidi ya yote, akimweleza hubby jambo hili ni wazi hata mimba hii anaweza kushtuka sio yake na ikawa shida kubwa kwangu.

Naombeni msaada kuhusu huyu msichana wa kazi nimfanyeje?
Nimechoka kuwa mtumwa, maana suala hili ni tangu December last year hadi sasa, utii wake umepungua sana, ni dharau tupu na nikimuona na wenzie wa hapa mtaani nakua na hofu sana kuwa atawapa umbea.

Sijawahi kuisaliti ndoa, safari hii ni huyu rafiki ndio alinirubuni tukaanzisha uhusiano huu, nilishindwa kukataa maana ndie mpenzi wangu wa kwanza na wa mwisho kabla sijaolewa sijui tulianzishaje suala hili.

Nimesitisha uhusiano nae since January, ingawa ananisumbua, mimba sijamweleza hivyo hajui.

Naomba mnishauri jinsi ya kumaliza hili tatizo.

Nitashukuru.
 
Kwa kweli jambo hili ulilianzisha mwenyewe kwa tamaa zako mwenyewe,ili kujiondoa na balaa hili,kwanza mwambie mume wako na utubu kweli kweli mbele ya mumeo na mbele za Mungu,ili ukabiliane na adhabu yoyote inayokupata. Kuendelea kumhonga house girl ni kuficha uovu kwa kitambo tu,lazima ipo siku atatoboa siri. Hivyo ni bora ukatubu mwenyewe. Kuna hatari kubwa sana inaweza kukufanya uwaze kumwangamiza housegirl wako. Kwa sasa huna hakika kabisa kama ameshawaeleza watu wengine. Ili usiendelee kutenda dhambi tubu kwa mumeo unaweza iokoa ndoa yako
 
Ngoja nikushauri tafuta namna ya huyo hg kuonoka hapo nyumbani kwa namna yeyote ile .. Kumbuka utajifungua halafu hg sidhani kama ataweza kulea huyo mtoto zaidi atakusumbua .... Matokeo ya ulichokifanya lazima ukubaliane nayo..

Nisingependa kuhukumu wala kukulaumu ila nina haya ya kukushauri na kushauri wanawake wenzangu.

Tuna katabia cha kushindwa kuacha marafiki wa nyuma hasa wa jinsia tofauti.. Kuachana au kupunguza marafiki pale unapoingia kwenye ndoa ni jambo gumu kufanya hasa kama unaogopa lawama.. Ni bora kutokuwa na marafiki wa karibu kiivyo mpaka mnaleta mazoea ya kuja home au kukutana maeneo ya starehe mara kwa mara hili litaokoa ndoa nyingi sana.....

Tuna msemo tunasema kwani alinikuta sina marafiki? Tujitahidi kupunguza mambo amabayo si ya msingi katika future ya ndoa zetu na watoto wetu, tumekuwa waroho na uchu wa kufanya ngono tena ngono zembe kwa visingizio vizivyokuwa na tija ooh aniridhishi ,.. oohh uume mdogo .. oooh sijui amenilaghai.

Hivi kweli mpaka umeolewa, bahati nzuri now days tunakuwa tumetembea na wanaume kabla ya ndoa, sasa hicho unachokitafuta kipya ni kipi hasa?

Jamani tuache kutesa na kusumbua hawa malaika, ni bora kutokuolewa kabisa ukaishi single milele utatiana na kila sampuli unayotaka mpaka kaburini lakini tusiwe chanzo cha kuwatesa hawa viumbe tena kwa sababu ya dushelelelee!
 
ngoja nikushauri tafuta namna ya huyo hg kuonoka hapo nyumbani kwa namna yeyote ile .. kumbuka utajifungua halafu hg sidhani kama ataweza kulea huyo mtoto zaidi atakusumbua .... matokeo ya ulichokifanya lazima ukubaliane nato,.........

nisingependa kuhukumu wala kukulaumu ila na haya yakukushauri na kushuri wanawake wenzangu tuna katabia cha kushindwa kuacha marafiki wa nyuma hasa wa jinsia tofauti .. kuachana au kupunguza marafiki pale unapoingia kwenye ndoa ni jambo gumu kufanya hasa kama unaogopa lawama.. ni bora kutokuwa na marafiki wa karibu kiivyo mpaka mnaleta mazoea ya kuja home au kukutana maeneo ya starehe mara kwa mara hili litaokoa ndoa nyingi sana..... tunamsemo tunasema kwani alinikuta sina marafiki? tujitahidi kupunguza mamabo amabayo si ya msingi katika future ya ndoa zetu na watoto wetu tumekuwa waroho na uchu wa kufanya ngono tena ngono zembe kwa visingizio vizivyokuwa na tija ooh aniridhishi ,.. oohh uume mdogo .. oooh sijui amenilaghai hivi kweli mapaka umeolewa bahati nzuri now days tunakuwa tumetembea na wanaume kabla ya ndoa sasa hicho unachokitafuta kipya ni kipi hasa? jamani tuache kutesa na kusumbua hawa malaika ni bora kutokuolewa kabisa ukaishi single milele utatiana na kila sampuli unayotaka mpaka kaburini lakini tusiwe chanzo cha kuwatesa hawa viumbe tena kwa sababu ya mbooooooooooooo......
Umeongea vizuri.. Ila Huku sio lile jukwaa Letu madam.
 
Hii kweli ni Into the Badlands, haya mambo ya mabadiliko ya Dunia yamefanya kila kitu kiwe vagalavagala. Hapo tunamaliza na kumsingizia shetani, wanadamu tunatenda mambo mpaka shetani anatushangaa tena.

Chamsingi pambana tuu mama na huyo house girl, ikiwezekana muondoe hapo home au kama vipi beba vyako ukagunge ndoa na yule jamaa ambae keshakutia mimba mpya.
 
na mimba umebeba jaman wanaume tunashida sana kwahyo senetnsi nyepesi umepigwa mbich na bado ukamwagiwa mweee.... kuna vitu viwil either uwe mkwel wa nafsi tu ila nalo gumu maana huyo hg atakunyanyasa maisha yako yote...
 
Back
Top Bottom