Dada anusurika kufa kwa kujitupa baharini leo akitoka Dar kwenda Zanzibar

RealTzboy

Senior Member
Jan 3, 2017
158
201
Huyo mwanamke ameokolewa kutoka baharini baada ya kujitupa kutoka kwenye boat leo wakati wakitokea Dar kuja Zanzibar. Tukio hilo limetokea maeneo ya Chumbe. Bado haijafahamika lengo na dada huyo kujitupa kwake kulikua na lengo.

Alikuwa akisafiri na boti ya Azam Marine Kilimanjaro V toka Dar kwenda Unguja ameopolewa baada ya kujirusha baharini. Taarifa za awali zinadai kuwa, hakutaka kurejeshwa nyumbani kwao Unguja. Mjomba wake alikuja kumchukua Dar ili kumrejesha Unguja

======

Taarifa Kutoka Kampuni Ya Azam Marine And Kilimanjaro Fast Ferries:


Kwa taarifa tu, abiria huyo alijitosa majini kutoka kwenye chombo chetu cha KILIMANJARO 5 maeneo ya Chumbe na taarifa zilipofika kwa Captain wetu, chombo kilipunguza speed na kurudi kwa ajili ya uokozi. Tulifanikiwa kumuokoa abiria huyo akiwa mzima na tumemkabidhisha kwa vyombo husika tulipofika bandarini Zanzibar.
 
IMG-20170403-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom