Cutting off Aid- a condition to lift Africa from Poverty?

najiulizana sana kwamba endapo misaada ya kigeni itasitishwa:

a. tutaendelea kuwa na NGOs nyingi hivi?
b. Je watanzania wanaweza kujitolea fedha zao kufanya kazi za kujitolea?
c. Itakuwaje kwenye misaada ya visima iliyoanzishwa na fedha za wahisani, tutamudu kuiendeleza?
d. Vipi kuhusu miradi mingine inayosapotiwa na wahisani nayo itakuwaje?

Mkuu MM, endapo misaada itasitishwa, nadhani

a. NGO nyingi zitakufa. Lakini labda tujiulize, NGO hizi zinafanya nini na kwa maslahi ya nani? Maana nyingi ya NGO zilizopo hazina manufaa ya kutosha kwa wananchi zaidi ya kujitwalia fedha nyingi za wahisani na kuzitumia kidogo katika miradi waliyoibuni. Maana yake ni kuwa, nyingi ya NGO zilizopo ni WIZI MTUPU.
b. Mkuu, watanzania wanaouwezo mkubwa wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo yao. Mfano; Unajua ukitaka kujenga barabara ya lami kwa fedha zako serikali haikuruhusu (hata kama ukifuata specs za serikali kujenga)? Sasa mambo kama hayo yangewekwa wazi na watu wakashiriki katika kujiletea maendeleo yao, nadhani nchi hii ingekuwa tofauti kabisa. Kinachihitajika ni serikali kutoa mwanya wa wananchi kushiriki katika mipango ya maendeleo kwa pamoja na serikali.
c&d. Kuhusu visima na miradi mingine iliyoanzishwa na wahisani, serikali inabidi ianze kujijengea uwezo wa kuitunza

Lakini yote hayo yatahitaji muda kwa kuwa ulemavu wetu katika misaada umekithiri. Itachukua muda na ujasiri wa kujitolea sana ili kuweza kufikia malengo bila misaada.
 
aisee huu mjadala ulikuwa mtamu sana! mwenye link ya article aliyoandika yule dada wa Zmbia Tafadhali anisaidie. Thanks
 
Haya ya MCC yalijadiliwa sana humu!

Angalizo lilitolewa mapema kuwa Misaada sii dawa ya kutuondoa kwenye umaskini Tanzania!

Yabidi tu tusimame kwa miguu yetu!
 
Hakuna nchi imepunguza, licha ya kuondoa umaskini kwa kupitia misaada. Misaada ni mazalio ya uzembe na kubweteka! Unafikiri kina Mkullo wanawaza sana jinsi ya kuongeza pato la ndani? Wanafanya upembuzi wa kina kutafuta vyanzo badala vya kuongeza pato? Kwanini wasumbue akili zao wakati kuna mahali "wataonewa huruma" watarushiwa 40% au which ever %!

Na tusisahau misaada hii hawana mtu wa kuwawajibisha nayo...mkiuliza mnaambiwa si kodi yenu! Lakini ni umaskini wenu, % za wasiofikiwa na huduma za afya, elimu, na social service zitakazowafurahisha donor na picha za kusikitisha za watanzania walala hoi zinatumika kuomba misaada hii. Hata watu wakikwepa kulipa kodi kwao ni ahueni ili wasibanwe na kuwajibishwa. Wapo tayari kujibu kwa donors na si kwa waliowaweka madarakani! Nguvu ya kisiasa wananchi wanayo pale tu wanapowapigia kura baada ya hapo wapiga kura wao wanageuka donors wanawajibika kwao si kwa watanzania

Misaada ni laana

Misaada inasababisha uzembe na kubweteka. Hili nakubaliana nalo kwa asilimia 100.
Chukuwa mfano mdogo tu. Wewe uko mjini, una maisha yenye hauweni. (you can pay your bills). Halafu pale kijijini kwenu umemuacha mdogo wako au wadogo zako ambao nao wanafamilia. Kwa sababu maisha uliyokulia unayajua usingependa kuona wadogo zako ambao hawakubahatika wakipata shida. Utaanza kuwapa misaada ili angalau waboreshe hali zao za maisha pale kijijini. Cha kushangaza, badala ya hiyo pesa unayowasaidia itumike kwa malengo yaliyokusudiwa, Wao unyea pombe na hata kuongeza mke wa pili au watatu. Suala la kulima au kujishughulisha wao huweka pembeni kabisa wakijua baada ya muda wakiomba misaada utawapatia.

Ndivyo ilivyo hata kwa misaada tunayopokea kama taifa kutoka kwa donors. Misaada hii imetufanya tubweteke na tusiwajibishane pindi inapotumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
 
Haya ya MCC yalijadiliwa sana humu!

Angalizo lilitolewa mapema kuwa Misaada sii dawa ya kutuondoa kwenye umaskini Tanzania!

Yabidi tu tusimame kwa miguu yetu!
Ni kweli yatupasa kusimama wenyewe lakini ni muhimu kuwa na mipango, tuache porojo na kudanganyana. Nia ya mheshimiwa Magufuli ni nzuri saaaaaana na naiunga mkono lakini tuwe na mipango, nchi haijitegemei.kwa kutumbuana majipu bali kwa sera na mipango madhubuti na endelevu.
 
Yawezekana nchi inayopokea misaada mingi ya kigeni kuwa na corruption ya kiwango cha juu? kwanini?
Dambisa Moyo, mchumi mkongwe wa Havard na raia wa zambia anasema kuwa nxhi zinanzopokea misaada sana inashindwa kuwajibika kwa wananchi wake. Pili inaonekana pia nchi kama hizi huwa watu wake hawalipi kodi inavyostahiki.. hivyo inakosekana check and balance mechanism. Wananchi wanashindwa kuiwajibisha serikali sababu hawana uchungu na pesa za kodi.. hivyo corruption inakosa muangalizi sahihi
 
Back
Top Bottom