TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,674
- 1,572
Chama cha Wananchi (CUF) kimeuweka rehani ushindi wa mbunge mteule wa Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Issa Mangungu, baada ya kufungua kesi kikipinga matokeo yaliyompa ushindi huo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2015 ilifunguliwa jana na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia CUF, Kondo Bungo, dhidi ya Mangungu, Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer- RO) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Hiyo ni kesi ya kwanza ya uchaguzi kufunguliwa kupinga matokeo ya ubunge kwa majimbo ya Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo, Bungo anapinga matokeo yaliyompa ushindi Mangungu, huku akiiomba Mahakama Kuu itamke kuwa uchaguzi huo ulikuwa batili.
Miongoni mwa madai yake ni kwamba uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi na ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), na kwamba ukiukwaji huo wa sheria umeathiri matokeo ya uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa hati ya madai yake aliyoiwasilisha mahakamani hapo, Bungo anadai kuwa mdaiwa wa pili (RO) alimteua na kumpangia kituo cha uchaguzi katika vituo vya upigaji kura, kata ya Kiburugwa ofisa ambaye ni ndugu wa mdaiwa wa kwanza (Mangungu).
Bungo anadai kuwa ofisa huyo ambaye ni ndugu wa mdaiwa wa kwanza, aliendesha uchaguzi pasi usawa na hivyo kuathiri uchaguzi huo.
Vilevile, Bungo anadai kuwa RO aliunda na kutambulisha kituo hewa cha uchaguzi kilichoitwa Makuka Kusini 4A, katika Kata ya Mbagala Kuu, jambo ambalo liliathiri uchaguzi.
Bungo anaendelea kudai kuwa RO na wasaidizi wake kinyume cha sheria waliruhusu mabango ya mdaiwa wa kwanza kubakia katika vituo vya kupigia kura vya kata za Kiburugwa, Tuangoma na Mbagala Kuu, licha ya malalamiko ya mawakala wake.
Chanzo: Mwananchi