Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtolea uvivu Dk. Lu Youqing, Balozi wa China nchini Tanzania, aliyesifia uchaguzi wa marudio Zanzibar uliofanyika tarehe 20 Machi mwaka huu.
Abdallah Mtolea, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CUF Taifa, amesema chama chao kinaelewa kwamba nchi yeyote inayofahamu demokrasia, uhuru na haki haiwezi kusema uchaguzi wa marudio Zanzibar ulikuwa huru na wa haki.
“Kama kuna nchi inayoamini kuwa uchaguzi wa marudio ulioamriwa na Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ulikuwa huru na haki, basi nchi hiyo ina matatatizo ya kidemokrasia,” amesema Mtolea ambaye pia ni Mbunge wa Temeke.
Amesema CUF inaamini kwamba China imetoa kauli hiyo ili kulinda maslahi ya kiuchumi ya China na ya raia wa China waishio Tanzania. “Communist Party of China (CPC), chama kikongwe kinachotawala China, na CCM wamekuwa na uswahiba wa muda mrefu. Uswahiba huu umefanya China kuwa kipofu kuhusu mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu,” anasema.
“China inaamua kuunga mkono kukandamizwa kwa demokrasia nchini Tanzania ili kujikomba kwa Serikali ili waendelee kupata hisani zaidi kwa maslahi ya taifa lao,” amesema Mtolea na kuongeza:
“China inapata tenda kubwa za ujenzi nchini Tanzania. Mfano ujenzi wa barabara, ambazo nyingine zimeanza kuharibika, madaraja na majengo makubwa. Hata mradi wa kusafirisha gesi wamo pia.”
Hata hivyo ameitaka China iache kufumbia macho ukiukwaji wa demokrasia nchini kwa maslahi yao na kuitumia Tanzania kujinufasha kwa rasilimali zake bila kujali msingi wa amani.
Dk. Youqingalitoa alitoa kauli ya kubariki uchaguzi huo wakati alipokutaa na Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungno, na Mazingira, ofisini kwa waziri huyo jana.
Dk. Youqing alimwambia Makamba kwamba China inaamini kuwa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni Zanzibar ulikuwa huru na wa haki.
Source: Mwanahalisi Online