CUF: Hatutapotea kwenye Siasa Nchini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema uamuzi wa kutoshiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar hauwezi kukipoteza katika ramani ya siasa nchini.

Badala yake, kimesema umekiongezea heshima kwa maelezo kuwa “ni heri kushindwa kwa kutoshiriki kuliko kushinda katika uchaguzi usio wa haki na uliojaa ukiukwaji mkubwa wa Katiba sheria”.

Januari 28, mwaka huu, Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho lilitangaza msimamo wa kutoshiriki uchaguzi wa marudio na kutoa hoja 12 likielezea kuwa ni batili na hivyo kushiriki ni kuhalalisha haramu kuwa halali.

Uchaguzi huo ulifanyika Machi 20 na mgombea urais wa CCM, Dk Ali Mohammed Shein aliibuka mshindi kwa asilimia 91. Shein aliapishwa juzi.

Akizungumzia mwelekeo wa CUF baada ya kukosa nafasi zote za uwakilishi, udiwani na urais, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Omary Ali Shehe alisema hakuna mwanachama wala mgombea atakayetetereka kwa kuwa wanajivunia uimara wa uongozi na msimamo wa wanachama.

Alisema CUF imejipanga kuendelea kujijenga kwa sababu lengo ni kuongoza nchi na kwamba, matokeo ya uchaguzi huo hayawatishi wala kuwayumbisha, badala yake yamewaimarisha zaidi.

“CUF haitakata tamaa mpaka pale ambapo CCM watajua maana ya siasa za vyama vingi na kuheshimu demokrasia. Tunajua athari ya kutoshiriki uchaguzi na tumepanga kuikabili hali hii, ila tungepata athari zaidi kama tungeshiriki,” alisema Shehe.

“Tutakachokifanya ni kurudi nyuma na kuanza kukijenga chama. Hatuwezi kuyumba wala kutetereka, maana hali kama hii imekuwa ikijitokeza lakini tunazidi kuimarika.”
 
who are they to decide their fate. wananchi wameshaamua kuwatosa. wamechoshwa na usanii wao. cuf imefikia tamati yake.
Nyinyi CCM mnajidanganya kupita kiasi.

Hivi mnadhani kwa kumtumia huyo Jecha wenu kuufuta ule uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 uliokuwa huru na haki kuwa ndiyo mtakuwa mmekiua chama cha CUF?

Badala ya CUF kudhoofika hivi sasa CUF ndiyo imekuwa more stronger.

Ukweli ambao haupingiki ambao dunia nzima inaujua hivi sasa ni kuwa Maalim Seif ndiye Rais wa Zenji kutoka mioyoni mwa wananchi wa huko na Dr Shein ni Rais aliyewekwa na vyombo vya usalama.
 
who are they to decide their fate. wananchi wameshaamua kuwatosa. wamechoshwa na usanii wao. cuf imefikia tamati yake.

KWA TAARIFA YAKO SASA, KWA MSIMAMO HUU MADHUBUTI WA CUF, SIKUWA NA CHAMA, LAKINI HATA MIMI SASA NITAJIUNGA NACHO NA NITAKUWA VOCAL NA KUHAMASISHA WATANZANIA WENGI. TUTAKUTANA MIAKA KADHAA.
 
CUF, kubalini mmeshindwa, maalim serf akubali amechoka kisiasa hana jipya, ajiweke pembeni, maalim pisheni msizibie wengine, chokochoko za nn,
 
Kwa uchaguzi ambao mwenyekiti wa tume anachaguliwa na rais wa Zanzibar ambaye pia ndiye makamu mwenyekiti wa CCM,CUF hawatashinda nafasi ya urais milele.
 
Afadhali mrudi kukijenga chama sababu upinzani umekufa na hamna cha kutetea ndani ya jamii, nani vyema mkaanza wenyewe ndani kwa ndani kwa kuheshimu katiba yenu kwenye ukomo wa madaraka
 
Back
Top Bottom