madala mujipa
JF-Expert Member
- Feb 23, 2017
- 1,417
- 860
Salaam wanajamvi
Kwa tukio lilitokea kwenye mkutano wa CUF la kuvamiwa na kundi la watu na kupiga waandishi na wengine kukamatwa ni suala linalotatiza kidogo baada ya hapo kumetokea kambi tatu zilizohasimiana na kukizana maneno na kunyoosheana vidole,
Wa kwanza kuibuka ni kambi ya Lipumba ilioshutumu CHADEMA kuwa vijana 100 walitumwa na kiongozi wa CHADEMA kuvuruga mkutano, kundi la pili ni kundi la CHADEMA lililotuhumu kambi ya Lipumba kuhusika na tukio lile, kundi la tatu ni kambi ya Maalimu linaloilaumu kambi ya Lipumba kuwa limehusika na uvamizi huo, mfuasi mwingine ambaye aliibuka ni Mtatiro kwa kusema ni TISS ndio waliovamia mkutano bila kufanya uchunguzi.
Wengi hapa katikati tulitupia lawama idara ya usalama wa taifa kuwa inateka watu na kuvamia mikutano, na kutishia wengine,
Je waungwana kwa hili la kambi kutupiana mpira hatujaisafisha TISS na madudu yake na kuendelea na kuendelea kutekeleza yale wayafanyayo kwa mtego wa kuwa vyama vyenyewe vinahujumiana?
Angalizo: CUF mnakoelekea sipo malizeni tofauti zenu hakuna jirani wa kutatua mgogoro wenu