Crypto-Currency sasa rasmi Tanzania

Kichochoro

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2017
Posts
1,135
Reaction score
1,168
Wakuu Kama habari inavyosomeka ni miaka mingi kidogo imepita kwenye huu ugunduzi wa pesa mtandao yaan crypto currency Leo hii tarehe 13/6/2021 mh Samia Hassan suruhu amelihudubia taarifa katika ufunguzi wa bank kuu Kanda ya ziwa nakuongeza kuhamasisha MATUMIZI ya Crypto-Currency.
===
Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kujiandaa na matumizi ya Sarafu za Mtandao (Crypto-Currency)

Amesema ni vyema BoT ikajiandaa kwa maendeleo hayo ili yakija yakute nchi ipo tayari

Ameongeza kuwa nchi inaweza kuona haiko tayari lakini Wananchi wakaitaka na wakawa wanaenda nje za nchi kupata huduma hiyo
 
Ungeandika vizuri basi?
 
"Amelihudubia taarifa" ulikuwa unawahi uwe wakwanza kuandika ona sasa,punguza mbio zisizo na malipo.
 
Nipo Muyama sijui inafanyaje kazi nami nawezaje kunufaika nayo huku kijijini
 
Mi sielewi,Mbona kama aina ya Kamari Iliyoboreshwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…