Wapendwa wana Jamvi,
Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.
Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?
Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.
Tiba
Binafsi pia sijawahi kufanya nao biashara,ninachokifahamu ni kwamba,kwakua wanamawasiliano na wewe watakupigia sim kila mara kuulizia umefikia wapi,kwa kweli inahitaji uvumilivu sana mana ni wasumbufu.
Nimewahi kufanya biashara na kampuni nyingine inaitwa Beforward,jamaa wako smart sana.
Mkuu magazeti yanaizungumzia hii kampuni? Au sijakuelewa.
Tiba
Nilikuwa naagiza gari mwezi wa kwanza nikachagua gari wakaniambia nina bahati kwa kuwa stock niliyochagua ipo baharini inakuja bandari ya Dar hivyo haitanichukulia muda sana. wakanipa na Bill of lading kumbe wametwist dates kwenye ile soft copy ya BL. Nilipokwenda kwa rafiki yangu ni clearing agent akacheki na TRA kumbe ile gari ilifika bandarini siku nyingi na ina port charges kibao. Ni jana tu nimeona kwenye gazeti TRA wanapiga mnada magari yao
The Pakistani are bad news, for what I hear. Kwanini usiongee na beforward?
Mkuu Tougher, asante kwa ufafanuzi. Ina maana waliokufanyia hivyo ni hawa hawa SBT Japan au ni kampuni tofauti. Inaelekea hawa SBT hawana ofisi Tanzania. Nipe ufafanuzi wa ziada mkuu.
Tiba
SBT Japan tatizo lao kubwa ni kwamba wanapakia gari zao kabla hata hawajapata wateja na zinafika bandarini wanaanza kusumbua wateja, mm mwenyewe walishapiga sana cm mpk ck hz ctak hata kuzipokea, hawajajipanga sawasawa bado!
SBT Japan tatizo lao kubwa ni kwamba wanapakia gari zao kabla hata hawajapata wateja na zinafika bandarini wanaanza kusumbua wateja, mm mwenyewe walishapiga sana cm mpk ck hz ctak hata kuzipokea, hawajajipanga sawasawa bado!
Tiba
Ni wao wenyewe nilikuwa nawasiliana nao toka huko, i have emails to confirm. Nilikuwa robo saa away from kuingia mkenge, nilikuwa nawasilian na mtu anaitwa Obadia Zia, nilipochomoa akaja huyu Hafiz Ishaq Ahmed, baadae tena akaja huyu Muhammad Ilyas. Walipoona nazidi kuwakatalia wakamleta huyu mwenye jina kama la kibongo Pete Andrew Cariaga.
[/TABLE]
Asante mkuu nashukuru kwa mchango wako. Sasa wakipakia gari kabla halijapata mteja likifika Bandarini inakuwaje? Wana agent wao hapa Tanzania kweli?
Tiba
yah..hawa jamaa kweli ni kampuni ipo na inauza magari na ndege pia. ni kubwa tu but wana tatizo moja na ucheleweshwaji wa kusafirisha gari. Mwaka jana nilinunua gari tika kwao gari ilkaa miezi mitatu ndio ikafika ikiwa haina spea tairi na betri imekufa. So for advice go to another company. Be foward ni wazuri kiutendaji but magari yao yanamikwaruzo sana na yameenda mileage kubwa.
kuna kampuni inaitwa tradecarview wako vizuri sana. nimefanya nao kazi mara mbili bila tatizo lolote.
I hear jamaa wa Pakistan wanatabia ya kukupa gari tofauti na walilokuonesha kwa picha na specs.Ndio mkuu Abdulhalim, hawa jamaa kama sio wahindi, basi ni wapakistani kwa muonekano wao na lafudhi yao. Be forward hawana hilo gari ninalolitaka kwa sasa. Kwabhiyo mkuu unsnishauri niachane nao hawa jamaa?
Tiba