CRDB tawi la Kaliua rekebisheni hili

CRDB tawi la Kaliua rekebisheni hili

Paragumu

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2014
Posts
326
Reaction score
142
Crdb benki sisi ni wateja wenu na mnajua kabisa bila sisi wateja mambo yenu yatakwama, sasa hapa Kaliua hali ni tete hususani kwenye utoaji huduma.

Mfano ni leo tarehe 05.06.2023 hapa tawini kuna wateja wengi hasa kutokana na wananchi wengi kulipwa malipo yao ya fedha za tumbaku sasa chakusikitisha wateja tumejazana hapa kwenye foleni Teller yuko mmoja tuu. Tunaomba mrekebishe hii hali maana muda mwingi tunautumia hapa.

Kuna wazee, wamama, watu wenye ulemavu wote tumejazana hapa ni kama hamjali vile boresheni huduma wananchi tunapata taabu hapa Uongozi wa CRDB tusaidieni hili ni haki yetu kuhudumiwa kwa wakati na kuondoka kwenda kwenye majukumu mengine.
 
Hakuna huduma bora yoyote inayotolewa kwa mlaji na haya makampuni yenye asali ya Nchini mwetu.

Mara nyingi makampuni ya nje wako vizuri ila bahati mbaya wana matawi machache mikoani
 
CRDB benki sisi ni wateja wenu na mnajua kabisa bila sisi wateja mambo yenu yatakwama,sasa hapa Kaliua hali ni tete hususani kwenye utoaji huduma. Mfano ni leo tarehe 05.06.2023 hapa tawini kuna wateja wengi hasa kutokana na wananchi wengi kulipwa malipo yao ya fedha za tumbaku sasa chakusitisha wateja tumejazana hapa kwenye foleni Teller yuko mmoja tuu. Tunaomba mrekebishe hii hali maana muda mwingi tunautumia hapa.

Kuna wazee,wamama,watu wenye ulemavu wote tumejazana hapa ni kama hamjali vile boresheni huduma wananchi tunapata taabu hapa Uongozi wa CRDB tusaidieni hili ni haki yetu kuhudumiwa kwa wakati na kuondoka kwenda kwenye majukumu mengine.
Kwani hamjui benk ya wakulima
 
Mkitoa hela zote, na wao watajiendeshaje?, lazima awepo mhudumu mmoja au mtandao uzingue ili hela zenu ziende kwenye mizunguko mingine, waendelee kutengeneza riba. Ndivyo mfumo ulivyokaa.
Wako pale kwa ajili ya kutengeneza faida na si kwa kukuhurumia wewe.​
 
Siyo kwamba hawalioni hilo ila ni mpango wao iwe hivyo, deal done
 
Back
Top Bottom