Hawajafikia huko mkuu, wakijirekebisha kwenye eneo hilo wataendelea kuwa the Best!AFADHARI UMESEMA
crdb ni shida, hata lengo la mkopo linayeyuka kabla ya kupata fedha! WANACHANGIA UMASIKINI HAPA TZ.Wachunguzwe vigezo ili waungane na wenzao watano wale.
Hapana broo, vikoba nako kuna matatizo yake! Ni bora nianzishe savings kidogo kidogo ya nyumbani kuliko vikoba!
Benki ya CRDB ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri sana hapa Tanzania kibiashara. Maeneo ambayo benki hii iliboresha na kuwa ya kupigiwa mfano ni eneo la huduma kwa wateja haswa kipengele cha kuwajali wateja. Watu wengi walikimbia foleni za NMB hususani watumishi mbalimbali.
Kwenye upande wa mikopo CRDB ni miongoni mwa benki zinazotoa mkopo wa gharama nafuu (riba kidogo) ukilinganisha na benki nyingine hivyo kujipatia wateja wengi wanaohitaji mikopo. Hapo kwenye utoaji wa mikopo haswa kwa watumishi wa umma ndio eneo linaloonekana kuja kuwaharibia haswa katika ufuatiliaji kuanzia kujaza fomu hadi kupata mkopo husika.
Imetokea mara nyingi mteja anajaza fomu za maombi anakabidhi Tawi husika kwa wakati lakini inachukua hadi miezi mitatu kwa fomu hizo kupelekwa makao makuu ya CRDB na baadae kwa mwajiri ili kupitishwa kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.
Labda tatizo ni wahisika wa kitengo hicho cha kupeleka fomu hizo kwenye mamlaka husika kuamua kwa makusudi kutopeleka fomu hizo ili kuwepo kwa mianya ya rushwa au ni uzembe tuu katika uwajibikaji, hilo CRDB wanatakiwa kufuatilia ili waendelee kuwa benki pendwa hapa Tanzania.
Sina wasiwasi na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mkuu ndugu Charles Kimei, ila namwomba afuatilie watumishi wake kwenye eneo hilo kabla ya kustaafu ili aondoke kwa heshima zaidi. Najua wahusika wapo huku hivyo naomba wampelekee maoni haya ili pafanyiwe marekebisho.
CRDB benki yangu.!
Hahaha zamani hata mimi nilidhani mabenki yana mashine za kutengeneza pesa. Sikujua kumbe pesa za bank ni accumulation za vijisenti vyetu. Jinsi wale wahudumu wanavyoringa pale mbele madirishani, nilikuwa nadhani wana print pesa kutugawia hahaha kumbe eti pesa yetu ndio inawaweka mjini lakini wanavyoringa.Kutengeneza brand huchukuwa muda sana ila kuporomosha ni fraction of a second!
Shida za mabenk yote tz zinafanana ila huwa zinatofautiana muda wa kutokea kwa watejaBenki ya CRDB ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri sana hapa Tanzania kibiashara. Maeneo ambayo benki hii iliboresha na kuwa ya kupigiwa mfano ni eneo la huduma kwa wateja haswa kipengele cha kuwajali wateja. Watu wengi walikimbia foleni za NMB hususani watumishi mbalimbali.
Kwenye upande wa mikopo CRDB ni miongoni mwa benki zinazotoa mkopo wa gharama nafuu (riba kidogo) ukilinganisha na benki nyingine hivyo kujipatia wateja wengi wanaohitaji mikopo. Hapo kwenye utoaji wa mikopo haswa kwa watumishi wa umma ndio eneo linaloonekana kuja kuwaharibia haswa katika ufuatiliaji kuanzia kujaza fomu hadi kupata mkopo husika.
Imetokea mara nyingi mteja anajaza fomu za maombi anakabidhi Tawi husika kwa wakati lakini inachukua hadi miezi mitatu kwa fomu hizo kupelekwa makao makuu ya CRDB na baadae kwa mwajiri ili kupitishwa kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.
Labda tatizo ni wahisika wa kitengo hicho cha kupeleka fomu hizo kwenye mamlaka husika kuamua kwa makusudi kutopeleka fomu hizo ili kuwepo kwa mianya ya rushwa au ni uzembe tuu katika uwajibikaji, hilo CRDB wanatakiwa kufuatilia ili waendelee kuwa benki pendwa hapa Tanzania.
Sina wasiwasi na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mkuu ndugu Charles Kimei, ila namwomba afuatilie watumishi wake kwenye eneo hilo kabla ya kustaafu ili aondoke kwa heshima zaidi. Najua wahusika wapo huku hivyo naomba wampelekee maoni haya ili pafanyiwe marekebisho.
CRDB benki yangu.!
Hahaha zamani hata mimi nilidhani mabenki yana mashine za kutengeneza pesa. Sikujua kumbe pesa za bank ni accumulation za vijisenti vyetu. Jinsi wale wahudumu wanavyoringa pale mbele madirishani, nilikuwa nadhani wana print pesa kutugawia hahaha kumbe eti pesa yetu ndio inawaweka mjini lakini wanavyoringa.
Nilifanya uamuzi ili kutokukerwa na hao waudumu siweki pesa bank hakuna faida yoyote. Maana hata usipokuwa na pesa ukitaka mkopo unapata tu. Hahaha siku nikizifuma natengeneza mto nalalia sitaki usumbufu na brand zenu. Mara CRDB, CCBRT, sijui UVCC, CCM mi nikiona "C" basi napita kushoto sitaki shida kabisa.