getwaa
Member
- Jul 28, 2015
- 42
- 17
Benki ya CRDB ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri sana hapa Tanzania kibiashara. Maeneo ambayo benki hii iliboresha na kuwa ya kupigiwa mfano ni eneo la huduma kwa wateja haswa kipengele cha kuwajali wateja. Watu wengi walikimbia foleni za NMB hususani watumishi mbalimbali.
Kwenye upande wa mikopo CRDB ni miongoni mwa benki zinazotoa mkopo wa gharama nafuu (riba kidogo) ukilinganisha na benki nyingine hivyo kujipatia wateja wengi wanaohitaji mikopo. Hapo kwenye utoaji wa mikopo haswa kwa watumishi wa umma ndio eneo linaloonekana kuja kuwaharibia haswa katika ufuatiliaji kuanzia kujaza fomu hadi kupata mkopo husika.
Imetokea mara nyingi mteja anajaza fomu za maombi anakabidhi Tawi husika kwa wakati lakini inachukua hadi miezi mitatu kwa fomu hizo kupelekwa makao makuu ya CRDB na baadae kwa mwajiri ili kupitishwa kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.
Labda tatizo ni wahisika wa kitengo hicho cha kupeleka fomu hizo kwenye mamlaka husika kuamua kwa makusudi kutopeleka fomu hizo ili kuwepo kwa mianya ya rushwa au ni uzembe tuu katika uwajibikaji, hilo CRDB wanatakiwa kufuatilia ili waendelee kuwa benki pendwa hapa Tanzania.
Sina wasiwasi na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mkuu ndugu Charles Kimei, ila namwomba afuatilie watumishi wake kwenye eneo hilo kabla ya kustaafu ili aondoke kwa heshima zaidi. Najua wahusika wapo huku hivyo naomba wampelekee maoni haya ili pafanyiwe marekebisho.
CRDB benki yangu.!