CRDB mjirekebishe,Huduma zenu mbovu

CRDB mjirekebishe,Huduma zenu mbovu

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2010
Posts
230
Reaction score
57
Poleni na Majukumu wana JF,naandika waraka huu kuelezea masikitiko yangu kwa CRDB. Kwanza kabisa,mtandao wenu wa ATM ni korofi sana,na mara nyingi ATM zenu zinakuwa hazina pesa hata kama hiyo ATM ipo kwenye tawi,mfani pale brach ya Mlimani city pana ATM kama sita hivi na utakuta ni ATM moja tu ndo inafanya kazi na foleni ipo hadi getini,hivi ni kwamba hamjali au ndo uzembe kwa kuwa mnawateja wengi? maana juzi tulikaa kwenye foleni karibia nusu sa hadi tukawagongea Benki ndo wakajifanya wanajaza pesa na wakati huo huo hii mnayoita SIMBANKING mara nyingi network yake iko chini.

Pili, suala la huduma ndani ya benki ni mbovu,hili nililiona Mbeya na pia nimeliona hapa Dar es Salaam.Unaenda Bank unakuta kuna viosk vya wahudumu sema sita na ni kimoja au viwili ndo vinawahudumu,cha kuchekesha ni pale wahudumu hao wachache wanapokuwa busy na simu za saloon na shopping wakati foleni inasubiri huduma. Cha kusikitisha ni pale wahudumu wote wanapotoka kwenye viosk vyao bila hata kusema kunanini na kutuacha wateja tunashangaa tu,ndio kuna kunywa chai nk lakini kama wateja tunapaswa kuelezwa sababu ya wahudumu wote kutokuwepo vioskini mkizingatia matawi yenu Mengi hayana viti vya kukaa kusubiria huduma so muda mwingi wateja tunakuwa tumesimama.Ningewaandikia kwenye sanduku lenu la maoni lakini nimeshaandika zaidi ya mara kumi na hakuna kinachobadilika,labda kwa kuwavua nguo huku labda mtabadilika..Kwa lugha rahisi CRDB mnaboa sana,pesa kuweka foleni,kutoa foleni..Badilikeni
 
NI KWELI..!!! pale mlimani city zile ATM zote ni kanyaboya.., infact 90% ya muda huwa hazina pesa..! zile za ubungo ndo kabisa..., sijawahi kukuta pesa.., SIMBANKING ndio usiongee.., password inafanya kazi kwenye ATM lakini kwenye SIMBANKING naambiwa eti nimekosea password.., naona hata uvivu kwenda kuuliza juu ya hili..., inshort mnabweteka..!!!
 
upuuzi mtupu. wanakera sana. sasa kwanini wakajaza makaunta kibao si wayatoe
 
Back
Top Bottom