CRDB Geita, huduma ni mbovu jirekebisheni

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Jana nilikwenda kupata huduma katika CRDB Tawi la Geita. CRDB Geita ina wateja wengi sana na hii imetokana na Mgodi wa GGM kuwa maeneo hayo lakini huduma inayotolewa na Benki hiyo haina kiwango hata kidogo. Madirisha ya kutoa huduma ni kama matano hivi lakini madirisha yanayotoa huduma ni mawili tu na hii inapelekea mstari kuwa mrefu na mteja kupoteza muda wake kwenye mstari. Jana nimekaa kwenye mstari kwa muda wa saa moja na nusu. Pili sehemu ya kujihifadhi kwa wateja haipo. Jana niliulizia sehemu ya kujihifadhi nikaelezwa kuwa mpaka Meneja aulizwe ndipo uweze kupata ufunguo wa kwenda kwenye chumba cha kujihifadhi. CRDB Geita badilikeni na muende na wakati.
 
Back
Top Bottom