Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,322
- 33,127
CPU za Loongson zilizotengenezewa na China zaingia kwenye soko la kimataifa
China ilianza utafiti wa kutengeneza CPU ya Loongson mwaka 2001, na kufanikiwa kutengeneza CPU ya Loogson No.1 mwaka 2002. Tukio hilo limekomesha historia kuwa kompyuta zilizotengenezwa na China kutumia CPU zilizotengenezwa na nchi za nje tu. Baada ya hapo, China ilianza kufanya utafiti wa CPU ya Loongson No.2. Hivi sasa CUP ya Loongson No.2E imeanza kuzalishwa kwa wingi na kutolewa kwenye soko la kimataifa kwa kushirikiana na kampuni ya Micro Electronics ya ST ambayo ni kampuni maarufu sana katika sekta hiyo. Kazi ya utafiti wa CPU za Loongson inayofanywa na taasisi ya teknolojia ya kompyuta katika taasisi ya Sayansi ya China inaungwa mkono na serikali ya China, na fedha zote za utafiti huo zilitolewa na serikali. Taasisi hiyo ilianza utafiti huo mwaka 2005, mkuu wa mradi wa CPU ya Loongson Bw. Hu Weiwu alisema: "CPU ya Loongson No. 2E inachukua nafasi ya mbele duniani katika usanifu wake, CPU hiyo ni ya kwanza yenye uwezo mkubwa duniani isiyotengenezwa na Marekani na Japan. Kasi yake ya kuhesabu inaweza kufikia mara bilioni 4 kwa sekunde, pia inatumia nishati kidogo zaidi. Hivi sasa CPU hiyo imeanza kuzalishwa na kuuzwa sokoni." Imefahamika kuwa, ingawa CPU ya Loongson 2E si CPU ya hali ya juu kabisa duniani, lakini imefikia kiwango cha CPU ya aina ya Pentium 4 iliyotengenezwa na Marekani. CPU ya Loongson 2E Ikilinganishwa na Pentium 4, CPU ya Loongson 2E ina bei ya chini zaidi na inatumia nishati kidogo zaidi, hivyo inapendwa na makampuni mengi yanayotengeneza software na kompyuta. Hivi sasa bidhaa zilizotengenezwa kwa kutumia CPU ya Loongson 2E ni pamoja na kompyuta na mfumo wa kompyuta wa kwenye televisheni na gari. Katika eneo la software, makampuni mashuhuri yakiwemo Microsoft, Xinhua pia yamesaini mkataba kusanifu software husika zinazolingana na CPU hiyo. "Kompyuta hiyo ina uwezo mkubwa na inauzwa kwa bei nafuu, na inaweza kukidhi mahitaji ya kawaida ya kazi za ofisi na burudani, kama vile kazi ya kuhariri makala, kutuma barua pepe, kuonesha video na kusikiliza audio." Mkuu wa taasisi ya teknolojia ya kompyuta katika taasisi ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Li Guojie aliona kuwa, kufanikiwa kwa utafiti na kutolewa sokoni kwa CPU ya Loongson 2E kunaonesha kuwa China imepata maendeleo makubwa katika teknolojia muhimu ya sekta ya upashanaji habari. Bw. Li Guojie alisema: "hivi sasa kompyuta ya mezani na kompyuta ya laptop zinalenga kukidhi mahitaji ya watu wenye pato la juu, tunapaswa kutengeneza na kueneza kompyuta kwa watu kwenye pato la chini. Katika siku za baadaye, CPU ya Loongson inaweza kubadilisha muundo wa soko la CPU duniani. CPU ya Loongson itatoa mchango wa kihistoria katika kupunguza gharama za upashanaji wa habari duniani." Kwa kushirikiana na kampuni ya ST micro electronics, CPU ya Loongson yenye hakimiliki ya China itaenezwa kote duniani. Kwa mujibu wa mkataba kati ya taasisi ya sayansi na teknolojia ya China na kampuni hiyo, kampuni hiyo itawajibika na uzalishaji wa CPU ya Loongson 2E na kuieneza kwenye soko la kimataifa kupitia mtandao wa usambazaji wa kampuni hiyo. Kampuni ya ST micro electronics pia itailipa China mrahaba na sehemu ya pato linalotokana na mauzo ya CPU hiyo. Hii pia ni mara ya kwanza kwa teknolojia ya usanifu wa CPU ya China kutumika kwa kulipwa na kampuni kubwa za nje. "Kampuni ya ST micro electronics inafurahi kushirikiana na taasisi ya teknolojia ya kompyuta ya China, tungependa kuzalisha CPU ya Loongson kwa kutumia vifaa na teknolojia zetu. Tunajua mahitaji ya taasisi hiyo, tutakuwa wenzi wazuri wa ushirikiano." Baada ya Loongson 2E, China itaendelea kuendeleza CPU ya Loongson, mkuu wa mradi wa CPU ya Loongson Bw. Hu Wei alisema: "Usanifu wa CPU ya Loongson 2F utakamilika hivi karibuni, na inatarajia kutolewa sokoni katika nusu ya pili ya mwaka 2007. Ikilinganishwa na Loongson 2E, Loongson 2F ina uwezo mkubwa zaidi, na matumizi yake ya nishati yamepunguzwa zaidi." Aidha, China pia itaendeleza CPU ya Loongson No.3, na CPU hiyo itatumika katika server na kompyuta ya hali ya juu. |