Conte, uliweza kumuumba Costa mwingine juu ya nyama zake

Halidi Mtumbuka

New Member
Jun 10, 2017
2
1
CONTE, ULIWEZA KUMUUMBA COSTA MPYA JUU YA NYAMA ZAKE.

Asubuhi na mapema kibaridi kikiwa kinapenya ipasavyo juu ya ngozi yako. Macho yanatua juu ya kidirisha cha chumba chako, unafurahia kuona jinsi nuru taratiibu inavyochukua nafasi ya giza, moyoni unajisemea "ahsante muumba wangu kwa kuiona siku nyingine, naomba iwe na furaha kwangu". Kwa kuwa bado hakujapambazuka vizuri unaamua kuivuta shuka ili ikukinge na baridi la asubuhi ya siku hiyo. Kweli unafanya hivyo lakini kabla hujamaliza kufanya hivyo simu yako ya mkononi inaashiria kuna ujumbe mpya umeingia. Unaamua kuachana na zoezi la kwanza. Moyo ukiwa umeongeza kasi ya mapigo yake ndani ya sekunde, mkono wako wa kulia unatua juu ya simu yako kisha unaanza mchakato wa kuufungua ujumbe wenyewe akilini kuna mawazo ya aina mbili, huenda ukawa mbaya au mzuri. Neno la kwanza kukutana nalo ni "Hahari" likifuatiwa na jina lako kisha ujumbe ukiendelea "natumaini uko poa. Ahsante kwa msimu tuliokuwa pamoja, nikutakie kila la kheri kwa mwaka unaofuata lakini haupo kwenye mipango yangu". Sina hakika kama utauamini uwezo wako wa kujua kusoma lakini kijasiri unaamua kujibu kifupi tu "sawa".

Au ni mchana wenye hali ya hewa nzuri, mandhari mazuri, pengine unapata chakula cha mchana kilichoandaliwa kiustadi wa hali ya juu kiasi kwamba kila kiungo kinachohusika kinapata haki yake. Pua inanusa harufu nzuri, mate yanajaa mdomoni yakiwa kile kimeng'enya cha chumvi huku tumboni nako ile tindikali na vile vimeng'enya vingine vikiwa vinaandaliwa kwa ajili ya chakula hicho. Lakini ghafla unapokea ujumbe kama huo unaosomeka hapo juu. Haijalishi pia kama ni jioni au usiku. Kikubwa ni saikolojia yako kwa wakati huo itakuwaje? Hivi ndivyo tunavyopaswa kujiuliza juu ya Diego Costa baada ya kupokea ujumbe wa maandishi kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa kocha wake Antonio Conte. Haukusomeka tofauti na nilivyoandika hapo juu isipokuwa kwenye jina lako weka jina la Diego, kisha usome wote. Nafikiri kitu cha kwanza kama mwanadamu, Costa aliurudia tena ule ujumbe kabla ya kufikia maamuzi ya kujibu vile kwa kifupi. Hakuwa na njia nyingine rahisi zaidi ya kujibu vile.

Kwa wapenzi wa Chelsea kumbukumbu hizi zitatembea akilini mwao kila iitwapo leo juu ya Diego Costa. Aliwapa mataji. Aliwafungia mabao muhimu. Lakini kwa upande mwingine aliwasumbua sana. Aliwafanya waishi kwa presha sana kipindi kile walichokuwa na Jose Mourinho. Vichwa viwili vyenye mawazo yanayoshabihiana vilikutana sehemu moja kisha vikajenga hekalu lao, wakaishi humo kwa vituko, vurugu na kila aina ya utovu wa nidhamu. Kuna wakati baba alilazimika kupandishwa jukwaani kwa makosa yaliyostahili kukemewa na yeye mwenyewe. Mtoto naye ndani ya uwanja alifanya vituko vya makusudi kwa kuwa kuna mtu nyuma yake atamtetea. Mwisho wa safari walifika salama, baba na mtoto wote waliibuka mashujaa kila mmoja kwa nafasi yake. Mwaka uliofuata ulikuwa ni wa shida, mateso, dhiki na dharau. Hakuna aliyekumbuka tena zile raha walizokuwa nazo miezi michache nyuma. Costa huyu aliyeota mbawa zilizozifunika zile za Chelsea alitengenezwa na Mourinho kujiona hivyo ingawaje hata alipotoka hadithi haikuwa tofauti na hii. Ni ngumu sana kuiamini taswira ya paka ilhali ilhali uhalisia ni simba.

Pamoja na yote lakini Costa alikuwa na msimu mzuri sana mbele ya Antonio Conte. Conte alifanikiwa nusu kuibadili tabia mbaya ya Costa kisha akamwingiza kwenye mfumo wake ulioipa ubingwa Chelsea. Inawezekana tabia yake ya kutoheshimu mkataba wake na kwenda kufanya mazungumzo na wachina ndicho kilichomkasirisha Conte. Lakini ni kweli Conte hakuwa na njia nyingine sahihi ya kuipita juu ya Costa? Hiki ndicho bora kwa upande wake? Njia aliyotumia ilikuwa sahihi? Siku zote anayejuliza maswali ndiye mwenye majibu sahihi kuliko hata yule anayeulizwa. Kwanini? Muuliza maswali anayomajibu ya ziada kwenye maswali yake. Mimi, wewe na Conte sote tuna majibu sahihi juu ya hili. Ninachokiamini, Conte hakushindwa kumuumba Costa mpya juu ya mwili wa Costa huyu. Kama alivyoweza kuiamsha miguu yake iliyolala na kuuziba mdomo wake wa kulalamika uwanjani asingeshindwa pia kuimalizia kazi aliyokwisha kuianza, alikuwa anaweza. Kama ambavyo alivyoweza kumfanya Costa awe muhimu msimu uliomalizika, asingeshindwa kumfanya awe muhimu zaidi msimu ujao, lakini alitaka kutengeneza heshima kikosini mwake. Anataka kukitawala chumba cha kubadilishia nguo, isikike sauti moja tu, kisha wote waifuate hiyo. Asitokee yeyote kati yao mwenye nguvu ya kusimama na kubishana nayo. Conte anataka sauti yake itawale chumba cha kubadilishia nguo.

Tatizo linakuja kwenye njia aliyoitumia. Ilikuwa ngumu sana kwa upande wa Costa lakini hakuwa na namna kwani ni mpango ambao ulihitaji kuwafanya kina Romelu Lukaku wanaokuja wasijione wapo juu ya Conte na Chelsea. Hata Sir. Alex Ferguson alikuwa akiitumia njia hii katika kujenga nidhamu kwa kikosi chake. Ni hapo tunapoamini kwamba huenda ni njia sahihi haijalishi umuhimu, mchango wa Costa wala kiwango cha jasho alichovuja kwa miaka mitatu ndani ya dimba la Stamford Bridge. Ferguson hakumvumilia yeyote asiye na nidhamu, aliamini kwenye nidhamu. Huwezi kuwa mwenye daraja kubwa duniani bila kuwa na nidhamu. Ninamashaka sana na hii misimamo ya makocha, kuna wakati inawafanya wawe wa kipekee sana lakini kuna wakati hulazimika kupitia wakati mgumu wanapotekeleza majukumu yao, hebu mwangalie Pep Guardiola anapofanya uamuzi wa kumuacha Joe Hart. Uamuzi unaowachukiza Waingereza. Ingawa atakipata anachokitaka lakini si kwa asilimia zote, kama ambavyo Adolph Hitler alivyoshikilia misimamo yake ingawa alifanikiwa lakini si asilimia zote.

Wako;
Halidi Mtumbuka.
halidimtumbuka@gmail.com
 
NI AIBU KUMWONDOA MCHEZAJI MKUBWA KAMA COSTA KWA NJIA YA SMS.HII NI DHARAU NA KIBURI CHA HALI YA JUU
 
NI AIBU KUMWONDOA MCHEZAJI MKUBWA KAMA COSTA KWA NJIA YA SMS.HII NI DHARAU NA KIBURI CHA HALI YA JUU
Angefanya hivo Mourinho hiyo habari ingetangazwa hadi fox news na CNN ila kwa vile ni conte basi poa, wachezaji wengi pale Chelsea dhambi waliyomfanyia mourinho haitowaacha salama kila mmoja na wakati wake! Wasije kujiona wapo salama hawatoamini watakapokuwa na mwisho mbaya
 
ibrahimovic out man u costa nae out chelsea........ namuona kabisa harry kane akipiga hatrick ya ufungaji bora epl.
 
NI AIBU KUMWONDOA MCHEZAJI MKUBWA KAMA COSTA KWA NJIA YA SMS.HII NI DHARAU NA KIBURI CHA HALI YA JUU
69527040283c2f0196d19a1a8716d4e9.jpg



Kufikia hatua unajipangia muda wa kucheza ni dharau zaidi kwa Kocha, eti umpangie akutoe muda fulani hata hujaumia.
 
Ngoja amuondoe aliyesaidia kupat ubingwa wakifungwa nakupoteza ubingwa atamkumbuka kwani atatimuliwa pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom