Mtu ukitaka kuelewa serikali yetu hivi sasa ilivyo hadi kwa watendaji ni sawa na picha za Simba na Yanga za miaka hiyo ambapo unakuta kundi fulani la wachezaji ama hutii Dewji tu au Marehemu Abbas Gulamali, Tarimba, George Mpondela, au Rage kwa kutegemeana na nani aliyemuingiza mle.
Utii wa utumishi serikalini ni mparaganyiko kwa kwenda mbalee tena wengine ni hujuma ya juu kwa juu nyumba kudondoka yenyewe kwa mchu wa kutafuna chuma ambao ndio wengi zaidi waliomo huko.
Mambo si mseto tena serikalini, mambo ni mparaganyiko mtupu tangu ngazi ya kata hadi Magogoni; kula mmoja keshaanza kupiga darubini mbele kwa uhakika wa mabadiliko makubwa yanayoendelea kucheleweshwa na CHADEMA kutokea.