Coil za Engine ya Altezza 3Sge (G 4 Automatic) kutofautiana

Mtanzanika

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
2,389
1,131
Wakuu,
Nimekutana na changamoto hii kwa mara ya kwanza. Coil za engine tajwa hapo juu zimetolewa katika engine kama hiyo tuite Engine A zikawekwa katka engine nyingine kama hiyo tuite Engine B.

Chakushangaza katika Engine B hazifiti, yaani fupi kiasi kwa hyo hazichomi vizuri, wakati zimetolewa katika Engine A zikiwa zinafiti na kuchoma vizuri.

Tumejaribu coil za kibati na zile za plastic matokeo ni hivyo hivyo. Sasa tumefunga za plastic kwa kulazimisha tu lakini hazijafika katika point yake inayopaswa kufikiwa yaani bado fupi kidogo.

Mwenye uzoefu katika hili tafadhali naomba msaada.
 
Mkuu, 3S GE ya Altezza haiingiliani na 3S GE yeyote. Hiyo ni dual vvti, imetengenezwa kwa ajiri ya Altezza RS200 pekee. So kama unataka kubadilisha parts, hakikisha unatafuta ya Altezza RS200 pekee. Nyingine japo zina same name na muonekane kidogo ila ni engine tofauti.
 
Asante mkuu kwa maelezo yako. Nimeweka picha ili iwe rahisi kurejea ninachozungumzia. Picha niliyoweka ni 3sge ambayo naamini ni RS200. Sasa naomba kujua kama engine kama hii zinaweza zisiingiliane coils? Maana zote zinafungwa kwenye Altezza ambapo nikitoa coils huku nikaweka kule hazikubali.
 
Attachments

  • Toyota_3S-GE_(longitudinal)_001.JPG
    Toyota_3S-GE_(longitudinal)_001.JPG
    91.1 KB · Views: 12
Asante mkuu kwa maelezo yako. Nimeweka picha ili iwe rahisi kurejea ninachozungumzia. Picha niliyoweka ni 3sge ambayo naamini ni RS200. Sasa naomba kujua kama engine kama hii zinaweza zisiingiliane coils? Maana zote zinafungwa kwenye Altezza ambapo nikitoa coils huku nikaweka kule hazikubali.
Kama ukipata za 3sge ya RS200 zitaingiliana. Labda kuwe na ishu nyingine. Ikishindikana hapo basi tumia part number kutafuta ili upate ile ile kama uliyotoa.
 
Back
Top Bottom