Good People
JF-Expert Member
- Aug 6, 2016
- 945
- 1,819
Hatimaye Klabu ya Simba SC imelipa kodi iliyokuwa inadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya nyasi bandia walizokuwa wamezitelekeza bandarini mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.
Geofrey Nyange 'Kaburu'
Hatua hiyo imekuja baada ya TRA kutangaza kuzipiga mnada nyasi hizo endapo wangeshindwa kukomboa kwa siku 14 waliozokuwa wamepewa ambazo zilimalizika juzi Jumanne.
"Mpaka sasa tumeshalipia kodi yote ya nyasi bandia, kinachoendelea sasa hivi ni wakala wetu kumalizia taratibu za kutoa 'container' zenye nyasi hizo bandarini kwenda kuwekwa rasmi katika uwanja wetu wa Bunju". Alisema Makamu wa Rais wa klabu ya hiyo Geofrey Nyange 'Kaburu'.
Kwa upande mwingine klabu hiyo inaendelea kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Jumatatu ijayo.