Clouds 360 - Mchezo nna uzalendo

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,210
Nawapongeza clouds 360 kwa kazi nzuri - kipindi cha asubuhi kinachoishia saa nne asubuhi.
Jambo ambalo linanikera ni Bwana Tupatupa wa kipengele cha michezo.
huyu bwana anaweza kuamua muda wake wote aliopewa kuongelea habari ya tenis za Sweeden, basket ball ya Marekani, Table tenis za China, Kutereza barafu Greenland, yaani mambo ambayo hayasaidii kitu katika kuhamasisha na kuinua michezo ya hapa Tanzania au hata Africa.

Huyu kijana hebu mpe guidelines. Aongelee michezo mikoani, michezo kitaifa, michezo africa nadi aaendelee na matenesi yake ya ulaya.

Kuna wakati aliongelea Basketi ball za USA akaacha kabisa kuongelea michezo ya AFCON inayoendelea Gabon, wakati jana yake Uganda walikuwa mchezoni. Hepu arekebishe presentation yake.

Twambie michuano soka ya ligi ya akina mama imefika wapi, twambia habari ya Alfonsi alivyonyakua medali ya mbio huko India, twambie jinsi Serengeti boys wanaweza endelea na mashindano, twambie mpaka sasa AFCON timu ziko status gani, twambie taifa stars yawezaje kuinuka, twambie jinsi CCM wanataka weka nyasi bandia ktk viwanja vyote wanavyomiliki, Twambie serikali imepata kodi kiasi gani kutoka ktk viingili vya michezo, komaa kijana , au kama vipi andaa kiindi kabisa cha michezo cenye masiliano ya mja wa mja na wadau ili tuchangie mawazo yetu.
 
Peleka jukwaa la michezo, wengine hatufuatilii michezo
 
Mawazo mgando ,dunia ni kijiji na sio watu wote wanapenda football
Other wise msikilize Kitenge kule E Fm ni Simba na Yanga mtindo mmoja siku saba kwa wiki
 
Back
Top Bottom