CIA walisumbuka kuhusu mrithi wa Baba wa Taifa,1985

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
7,112
10,218
INADAIWA KUWA:
MAREKANI ilikuwa inasumbuka kuhusu mrithi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama Rais wa Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985, imefahamika.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) nani angemrithi Mwalimu Nyerere lilikuwa ni suala ambalo liliumiza vichwa vya taifa hilo tajiri duniani.

Kwa kawaida, CIA imekuwa na utaratibu wa kuweka hadharani baadhi ya siri kuhusu ujasusi wake katika mataifa mbalimbali duniani; lakini baada ya kipindi fulani kupita.

Safari hii, CIA imeweka hadharani siri za namna ilivyofuatilia matukio mbalimbali katika siasa za kitaifa za Tanzania; hususani mwelekeo wake endapo Nyerere angeondoka madarakani au angeendelea.

Kwa kawaida, ripoti hizo za CIA huwa zina ukweli ingawa wakati mwingine –hasa kwa taarifa hizi mpya za Tanzania, kuna maeneo ambako ubashiri wao unakuwa si wa kweli na upungufu mwingine katika usahihi wa majina ya wahusika.

Musoma Group

Taarifa hizi mpya za kijasusi, zinaonyesha kwamba kuelekea mwaka 1985 ambako Uchaguzi Mkuu ulikuwa umepangwa kufanyika, kulikuwa na hali tete kuhusu mwelekeo wa taifa.

Kwanza, nchi ilikuwa katika hali ngumu ya kiuchumi baada ya kumalizika kwa Vita ya Kagera na ilikuwa haieleweki kama Mwalimu ataendelea na urais au atamwachia mtu mwingine.

Ripoti hiyo ya kikachero ya CIA; shirika kubwa zaidi la ujasusi duniani, ilibainisha kwamba kulikuwa na kundi lililojiita Musoma Group lililoanzishwa kwa minajili ya kumbembeleza Mwalimu asiachie madaraka.
Ripoti ya kijasusi yafichua mazito mbio za urais – Raia Mwema
 
Back
Top Bottom