Mi naona huu ni uamuzi wa kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Hivi kweli tuna tatizo la wataalamu wa kilimo? Serikali haijui adha wanayopata wanafunzi wa SUA ktk soko la ajira?Kuna wanafunzi wengi wa SUA wako ktk mabenki na wengine ni waalimu wanafundisha shule za sekondari kwa leseni. Na wengine wapo tu mtaani, hii ina maana serikali inasomesha nguvukazi ambayo haitumiki ipasavyo. Serikali inapaswa kufanya utafiti kwanza kabla ya kuanzisha vyuo vikuu mbali mbali huku ikiviacha vingine yatima (kifedha). Kuna faida gani ya kuwa na vyuo vingi vilivyojaa maTA (ambao nao kimsingi ni wanafunzi), badala ya kuwa na vichache vyenye ubora wa miundombinu na wabobezi? Kupeleka Chuo Kikuu cha Kilimo Katavi ni kumfurahisha Ndugu Pinda kwa kuwa anapenda kulima.Nimestushwa na taarifa ya serikali kutaka kujenga chuo kikuu kingine cha Kilimo katika mkoa wa Katavi, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira la leo. Sababu ya mstuko huo ni hali mbaya ya vyuo vyetu vya kilimo vilivyopo ambayo vinashindwa kijikidhi na kutoa huduma stahiki kutokana na bajeti finyu inayopokea kutoka serikalini. Chuo kikuu kilichopo (SUA) bado kinahitaji kujitanua na hakijajitosheleza wataalamu, hivyo ni heri serikali ingeongeza nguvu kwenye chuo hicho kama inajali zaidi wakulima. Kwa miaka ya karibuni sasa kumekuwa na mfumuko wa vyuo vikuu Tanzania jambo lililopelekea hata kushusha viwango vya kuingia kwenye vyuo hivyo, jambo ambalo lilibarikiwa na Tume ya vyuo Vikuu (TCU). Mfumuko huu utasababisha kutozalisha wataalamu waendeshaji/ watendaji wenye ngazi ya Diploma na Cerificates ambao ni wanahitajika sana kutokana na mahitaji ya Taifa. Bado wataalamu wa Kilimo hawatoshelezi Kata zote nchini, licha kimfumo kila kijiji kinahitaji bwana shamba na bwana mifugo ambao vijiji vingi sana hawana, hivyo hata kupata maelekezo/ushauri wa kitaalamu haiwezekani. Sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kina katika kuwekeza kwenye mahitaji ya wataalamu wa kilimo nchini.
Vyuo vya Kilimo na Utafiti vya serikali ninavyovikumbuka kwa uchache, (wachangiaji mtanisaidia kuongezea vingine vingi):
- Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro;
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Uyole Mbeya
- Chuo cha maendeleo ya Mifugo Tengeru (LITI-Tengeru) Arusha
- Tengeru Horticultural Reasearch and Trainning (HORTI).- Arusha
- Chuo cha kilimo na Utafiti Kilombero (KATRIN) Morogoro
- Chuo cha Kilimo taaluma ya umwagiliaji Igurusi - Mbeya
- Chuo cha kilimo na Utafiti Ilonga (MATI Ilonga) Morogoro
- Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro (KATC) - Kilimanjaro
- Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Mlingo
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Morogoro (LITI Morogoro) Morogoro
- Chuo Cha Utafiti wa Kilimo Cha Ukiriguru
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Buhuri (LITI Buhuri) Tanga
- Chuo cha Maendeleo ya Kilimo Inyala Mbeya
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) Arusha
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Mpwapwa (LITI Mpwapwa) - Mpwapwa
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele Mtwara
- Chuo cha utafiti wa Kilimo Tumbi Kibaha
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Mlingano Tanga
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Tumbe Tabora
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa magonjwa ya wanyama (ADRI) DSM
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Madaba - Songea
Vyuo hivi vingeweza kutumika vizuri kufundisha wataalamu na hata wakulima ili kuweza kuendesha kilimo chenye tija. Tukumbuke kuwa, wananchi wengi maskini Tanzania ni wakulima, hivyo tukiacha hivi vyuo vijiendeshe kibiashara kama vyuo vya uhasibu ama IT ambavyo wahitimu wake ni rahisi kuajiriwa mijini. Vilevile mazingira bora ya watumishi wa vijijini yanahitajika ili kuwavutia wataalamu kufanya kazi vijijini. Kama serikali haitaweka kipaumbele kwenye kuboresha miundombinu vijijini na kuelimisha wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija ni dhahiri kuwa wimbi la vijana kukimbilia mijini halitakoma. Serikali ilitakiwa kuvisaidia kwa hali na mali vyuo hivi vilivyotawanyika nchi nzima japo vina wataalamu wachache bado. Sioni mantiki ya kukimbilia Kujenga chuo kikuu cha Kilimo Katavi wakati wahadhiri/watafiti hawapo wa kutosha nchini (SUA haijajitosheleza bado). Vilevile kwa Tanzania ya leo bado ni ndoto kuwa na mabwana shama wenye taaluma ya degree, hivyo ni vema tukaweka mkazo kwanza kwenye hivi vyuo vya diploma na certificate. Wakati utafika ambapo tutakuwa na hitaji la vyuo vikuu baada ya kujitosheleza kwenye hii ngazi ya kati kimahitaji. Swala la Chuo kikuu Katavi ni la haraka mno na linaonekana lina maslahi kisiasa zaidi kuliko kutoa huduma ya elimu, ushauri na utafiti kwa wananchi.
Nimestushwa na taarifa ya serikali kutaka kujenga chuo kikuu kingine cha Kilimo katika mkoa wa Katavi, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira la leo. Sababu ya mstuko huo ni hali mbaya ya vyuo vyetu vya kilimo vilivyopo ambayo vinashindwa kijikidhi na kutoa huduma stahiki kutokana na bajeti finyu inayopokea kutoka serikalini. Chuo kikuu kilichopo (SUA) bado kinahitaji kujitanua na hakijajitosheleza wataalamu, hivyo ni heri serikali ingeongeza nguvu kwenye chuo hicho kama inajali zaidi wakulima. Kwa miaka ya karibuni sasa kumekuwa na mfumuko wa vyuo vikuu Tanzania jambo lililopelekea hata kushusha viwango vya kuingia kwenye vyuo hivyo, jambo ambalo lilibarikiwa na Tume ya vyuo Vikuu (TCU). Mfumuko huu utasababisha kutozalisha wataalamu waendeshaji/ watendaji wenye ngazi ya Diploma na Cerificates ambao ni wanahitajika sana kutokana na mahitaji ya Taifa. Bado wataalamu wa Kilimo hawatoshelezi Kata zote nchini, licha kimfumo kila kijiji kinahitaji bwana shamba na bwana mifugo ambao vijiji vingi sana hawana, hivyo hata kupata maelekezo/ushauri wa kitaalamu haiwezekani. Sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kina katika kuwekeza kwenye mahitaji ya wataalamu wa kilimo nchini.
Vyuo vya Kilimo na Utafiti vya serikali ninavyovikumbuka kwa uchache, (wachangiaji mtanisaidia kuongezea vingine vingi):
- Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro;
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Uyole Mbeya
- Chuo cha maendeleo ya Mifugo Tengeru (LITI-Tengeru) Arusha
- Tengeru Horticultural Reasearch and Trainning (HORTI).- Arusha
- Chuo cha kilimo na Utafiti Kilombero (KATRIN) Morogoro
- Chuo cha Kilimo taaluma ya umwagiliaji Igurusi - Mbeya
- Chuo cha kilimo na Utafiti Ilonga (MATI Ilonga) Morogoro
- Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro (KATC) - Kilimanjaro
- Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Mlingo
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Morogoro (LITI Morogoro) Morogoro
- Chuo Cha Utafiti wa Kilimo Cha Ukiriguru
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Buhuri (LITI Buhuri) Tanga
- Chuo cha Maendeleo ya Kilimo Inyala Mbeya
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) Arusha
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Mpwapwa (LITI Mpwapwa) - Mpwapwa
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele Mtwara
- Chuo cha utafiti wa Kilimo Tumbi Kibaha
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Mlingano Tanga
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Tumbe Tabora
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa magonjwa ya wanyama (ADRI) DSM
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Madaba - Songea
Vyuo hivi vingeweza kutumika vizuri kufundisha wataalamu na hata wakulima ili kuweza kuendesha kilimo chenye tija. Tukumbuke kuwa, wananchi wengi maskini Tanzania ni wakulima, hivyo tukiacha hivi vyuo vijiendeshe kibiashara kama vyuo vya uhasibu ama IT ambavyo wahitimu wake ni rahisi kuajiriwa mijini. Vilevile mazingira bora ya watumishi wa vijijini yanahitajika ili kuwavutia wataalamu kufanya kazi vijijini. Kama serikali haitaweka kipaumbele kwenye kuboresha miundombinu vijijini na kuelimisha wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija ni dhahiri kuwa wimbi la vijana kukimbilia mijini halitakoma. Serikali ilitakiwa kuvisaidia kwa hali na mali vyuo hivi vilivyotawanyika nchi nzima japo vina wataalamu wachache bado. Sioni mantiki ya kukimbilia Kujenga chuo kikuu cha Kilimo Katavi wakati wahadhiri/watafiti hawapo wa kutosha nchini (SUA haijajitosheleza bado). Vilevile kwa Tanzania ya leo bado ni ndoto kuwa na mabwana shama wenye taaluma ya degree, hivyo ni vema tukaweka mkazo kwanza kwenye hivi vyuo vya diploma na certificate. Wakati utafika ambapo tutakuwa na hitaji la vyuo vikuu baada ya kujitosheleza kwenye hii ngazi ya kati kimahitaji. Swala la Chuo kikuu Katavi ni la haraka mno na linaonekana lina maslahi kisiasa zaidi kuliko kutoa huduma ya elimu, ushauri na utafiti kwa wananchi.
.......:...... True mkuu kwani umestukiaje kwamba son of a poor dad anashadadia kupata umaarufu wa milele...MKP UNIVERITY OF AGRICULTURE... P.O BOX 00000 MPANDA RUKWA... JIWE LA MSINGI LILIWEKWA MWAKA 2012 NA WAZIRI..........BW MKP....TU du mizengo bwana... Shabaabi kweli kweli wa umaarufu wakati mafisadi wamemweka kwapani anapelekwa kama bajaza..Pale wananchi watakapokuwa na nguvu ya kuamua pesa zao zitumike kufanya nini ndipo tutakapoachana na bajeti zinazofuata kuwapendezesha na kuwapa utukufu wanasiasa. Possibly kitaitwa Mtoto wa Mkulima University
badala ya kupongeza hatua nzuri tunaponda.....MIMI NAPONGEZA TENA VYUO VINGI ZAIDI VIANZISHWE ILI PIA KUJIJENGA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO TUTAKAZOKUTANA NAZO NA KUZITATUA