Chuo cha sayansi na teknojia Mbeya (MUST) ni mmoja wa chuo tulitarajia kitafungwa au kitazuiliwa kudahiri wanafunzi kama chuo cha St. Joseph na vyuo vingine hapa nchini lakini imekuwa tofauti sana labda huenda kwa sababu ni chuo cha serikali, serikali haitaki kufichua madudu yake katika taasisi zake za kutolea elimu na hiki hiki chuo kimejaa madudu mengi sana kinaishi bado kwa sababu ni cha serikali ila kingekuwa cha private kama St. Joseph kingeshafungwa muda.
Miundo mbinu ya chuo hiki ni duni kupindukia hakina hadhi ya kusimikwa kuwa chuo kikuu ni bora iwe taasisi kama hapo awali ilivyokuwa tena taasisi ya kutolea certificate ila sio diploma au degree, miundo mbinu kuanzia majengo, mabweni na madarasa hali ni tete na majengo haya yanatishia usalama kwa wanafunzi na tukumbuke huku mbeya kuna tetemeko la ardhi wiki chache nyuma tetemeko lilipita huku mbeya, je mnangoja wanafunzi wafe ndio mje kujenga chuo hiki na kukikarabati?
Chuo hakina maktaba ya kukidhi mahitaji ya wanafunzi vitabu hamna vya kutosha na maabara za hapa hazina hamna tofauti kama za shule za msingi au sekondari tena zinapitwa hata na zile maabara za shule za private, maktaba tunangoja ijengwe imekomea kwenye basement na ni takribani miaka Zaidi ya minne sasa. Bado hiki hiki chuo mnakiruhusu kianzishe fani za ualimu mnamo mwaka wa masomo 2017/2018 mnatarajia kitoe walimu wenye ufanisi wa kutosha.
Majengo na miundombinu ya chuoni hapa, vyote kwa ujumla vinaelekea kuwa kama magofu kama yale ya bagamoyo kwa kukosa ukarabati kwa muda mrefu pia ni miongoni mwa vyuo vinyaongoza kwa gharama kubwa ya michango, ada pendekezi ya TCU kwa engineering ni 1.1 million ukijumlisha na michango ya hapa chuoni ni jumla yake ni 1.55 milion kwa mwanafunzi wa bachelor degree hili ongezeko la laki nne linatoka wapi? Wakati Sokoine University of Agriculture (SUA) michango yao haizidi laki moja na nusu na vyote ni vyuo vya serikali na D.I.T pia gharama ya michango yao sio kubwa kama yetu, tunaomba serikali kwa ujumla na wizara ya elimu kwa ujumla mtusaidie hili swala naamini sio MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY pekeeake tu ndio wana tatizo hili la wanafunzi kutozwa gharama kubwa za pesa kuna vyuo vingine vipo, tunaomba wizara ya elimu, serikali kwa ujumla na TCU wapange bei elekezi hili swala likitekelezwa ipasavyo ada ya vyuoni itakuwa nafuu.
Tunaomba mnavyopanga bajeti ya wizara ya elimu mkumbuke kuna chuo huku mbeya kinaitwa MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY kinahitaji ujenzi au ukarabati wa hali ya juu, chuo kinahitaji maktaba, maabara,michango ipungunguzwe, vitabu vya kusomea, majengo mapya au yarekebishwe na pia vifaa vya kufundishia na pia utawala wa chuo nao sio mzuri kama ikiwezekana ubadilishwe tu.
Chuo kama chuo wanaeneno ni swala la kumtafuta mkandarasi na kumpatia pesa chuo kingine kijengwe au la sivyo kikarabatiwe hata kama hakina viongozi serikalini wametokea katika chuo hiki kikumbukwe tu maana tumeona kwa UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM (UDSM) kinapewa kipaumbele sana kwa sababu kimetoa viongozi wengi serikalini, hapo tunakuwa tunatengeneza matabaka, vyuo vyote vipewe hadhi sawa bila kujali chuo Fulani ni chuo mama Tanzania au kimeanza mwaka gani.
Na pia mjaribu kuja chuoni hapa mbeya mtembelee kila pembe ya chuo mtajua mapungufu ya chuo hiki kwa ujumla na mtathimini kama kina hadhi ya kusimikwa kuwa chuo kikuu au hiki na st.joseph ya dar kipi kilipaswa zuhuhiliwa kudahili wanafunzi katika mwaka 2016/2017 na kuendelea.
Kuna vyuo vingi hapa nchini vinahitajika kujengwa au kukarabatiwa hapa nchini kwa mfano huku mbeya chuo kama TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY-MBEYA CAMPUS ni mmoja wa chuo ambacho kinabidi kijengwe upya au kikarabatiwe upya maana miundo mbinu yake hayaendani sawa na matakwa au mahitaji ya elimu ya karne ya 21.
Tunanguvu kazi kubwa ikitumika ipasavyo taasisi zote za elimu hapa nchini zitajengwa na kukarabatiwa kwa gharama ndogo sana kwa mfano vijana wa JKT, vijana wale wanaoenda jeshini kwa mjibu wa sheria(form six), tuna wafungwa magerezani hii nguvu ngazi ikutimiwa ipasavyo hizi taasisi zote za elimu zitaboreshwa kwa gharama nafuu, hii nguvu kazi itumike kujenga taasisi hizi za elimu.
Pia tunaomba mthamini serikali za wanafunzi vyuoni mkishirikiane nazo mnaweza fichua madudu mengi katika vyuo vyetu hapa nchini, mkiendelea kutegemea feedback na report na management za chuo hazitasaidia kufichua mapungufu yalipo vyuoni lazima mshirkiane serikali za wanafunzi vyuoni.
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MAKTABA ILIYOPASWA
KUJENGWA NA IMEKWAMA KWA TAKRIBANI ZAIDI YA MIAKA
MINNE NA ZAIDI.
Mkifika chuoni hapa ndipo mtajua mapungufu ya hiki chuo, tunaomba mtume wakaguzi au waziri au katibu au naibu waziri au makatibu wengine wafike hapa chuoni pia hata sisi wanafunzi tutakuwa huru kujieleza matatizo yetu.
Huo muonekano wa chuo kwa aerial view si sawa na yaliyomo yaliyo ndani ya chuo.
Mwalimu mmoja analamika kufundisha wanafunzi Zaidi ya 200 kwa wakati mmoja bila kuwa sound systems za kufundishia hao wanafunzi mnatarajia wote wataelewa na kumsikia mwalimu?
Je kwa hali hii mnatarajia wanafunzi hao watapata motisha ya kuingia madarasani?
Nilichokiandika hapa sio takwimu au hadithi za kuasadikika na sio soga ni uhalisia wa chuo hiki cha MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY, mkifika mtashuhudia ukweli