dragon ball
Member
- Jul 17, 2015
- 57
- 4
Hlo nalo la kuleta huku?? Kwan hapo chuon hakuna wanafunzi wa mwaka wapili na tatu?
Mwandike email ya Malamiko Dr. Mganilwa, hicho chuo ni wazembe mno!Mimi ni mwanafunzi wa NIT wa mwaka wa kwanza ninayechukua bachelor ya Computer Science na bado hatujajua ratiba rasmi ya kozi yetu kwa semister hii had sasa.
Siku ya leo wenzetu wa IT wamepata ratiba yao yenye masomo manne ambayo Computing Mathematics,Fundamentals of computer,Computing and Applications n Programming principles. Tulivyoibuka stationery kuulizia ratiba wametuambia tutatumia ya IT kama ilivyo. Japokuwa ratiba ya IT imetoka leo lakini masomo hawajaanza kutokana na jengo linalotazamiwa kusomewa kutokamilika. Na inavyosemekana hata kesho itakuwa kuna ugumu vile vile.
Naomba kufahamu kwa waliotangulia ni kwamba kwa semister ya kwanza IT n CS huwa wanachanganywa na ratiba zinafanana au kwa sababu ya uhaba wa madarasa kwa NIT.
Na kama kuna mtu aliyemaliza Computer Science na ana full topics kwa 3 years aniorodhoshee nisome binafsi. Naona wanatuyeyusha hata kwenye profile zetu kwa tunaosoma CS hawajatuwekea ratiba....
Mwandike email ya Malamiko Dr. Mganilwa, hicho chuo ni wazembe mno!
We acha tu! Hapa sina muda niwahi kujiongeza nichukue mcheti wao...
Naona unataka kutumia style Ya Secondary kwa huko Chuo. Mkuu huwezi Pata Majibu Huku, hapo chuoni hamna viongozi wa kufuatilia?
Mkuu kwa kua uko CS, system ya bongo nilivyoipima miaka kadhaa naona bado iko shallow sana, hata maprofesa wenyewe wanahangaika mambo yanawasumbua, pepa zao nyepesi, hawagusii vitu advanced mwisho wa siku ukiishia wanachokufundisha peke yake utakua pabaya sana.
My suggestion anza kukimbiza mambo mwenyewe, soma ya darasani sawa lakini tenga masaa minimum matatu kila siku kuanzia leo hii hadi siku unagraduate, hayo masaa matatu chagua lugha moja mfano C, anza kufanya programming, hii ni kama kweli unataka kutoka vizuri kwenye hii industry, CS is more than programming, the main thing kwenye CS ni abstraction, unavoweza kubreak down matatizo yoyote yale unayokutana nayo na kuweza kuyasolve kirahisi in steps na more efficiently, ukiwa unasoma programming utakutana na almost kila kitu, utajikuta unasolve hadi matatizo yanayohusiana na kilimo, thats the beauty of it, inaapply kwenye field yoyote ile.
By mwaka wa tatu kama umefata hii ratiba utakua tayari umeweza kutengeneza your own apps ambazo zinaweza kukusaidia kupata hata internships kampuni za nje, India, Japan, US, UK pote kuna makampuni mengi yanatoa internships kwa international students ila kwa kua una~disadvantage tayari ya chuo ambacho hawakijui, apps ambazo utakua umefanya zitakunyanyua sana, wanajali sana projects zako kuliko grades za darasani au chuo ulichosoma. Naongea from experience.
Asante sana mkuu. Nitajitahidi kufanyia kazi kwa huu ushauri ulionipa...
Mkuu nimechagua kozi hii kwa kujikuta kuipenda programming language. Kuna video niliiona youtube wakiipigia promo kuhusu kujifunza Computer Programming huko USA. Wenzetu wana misingi mizuri kuanzia ngazi ya chini...You're welcome mkuu, I usually get excited kuona watu wanajaribu hii space coz mimi mwenyewe nimesoma CSE japo sio bongo, ni fied ambayo hata nikirudishwa chekechea am 100% ntaichagua tena coz nimejikuta natengeneza vitu ambavyo sikujua kama ntaweza tengeneza siku moja, nimeona watu pia wanaiparamia hii major vibaya mwisho wa siku wanaishia pagumu mno hawaoni manufaa yake, hawa ni wale wasiopenda kusoma kwa ajili ya knowledge wao wanasoma kwa ajili ya mitihani, sipendi kuona watu wanapotelea huko hasa mwaka wa kwanza ni mapema sana akienda njia sahihi anaweza akaanza kufanya vitu vya maana hata kabla hajagraduate.
Tanzania inakua sasa hivi tunahitaji sana watu kwenye technology ambao wako fit, its the only way forward kama we also want to stand out kwenye world market.
Also, find someone muwe mna~program pamoja, dont do it on your own kwa kujifungia, that way it will be fun, ikifika muda anzeni kutengeneza virobot vidogo mnavipiganisha..
We acha tu! Hapa sina muda niwahi kujiongeza nichukue mcheti wao...
Acha kiwewe degree aitafutwi kwa mbwembwe anachokufundisha dk nicho unachotakiwa kujibu na nicho unachotolewa kwenye test na UE,semister hii lazima niwale vichwa.
Kashakuwa Prof. siku hizi, alinifundisha engineering design, ni mtu makini sana sielewi hii hoja ya mleta mada kama ina ukweli.Mwandike email ya Malamiko Dr. Mganilwa, hicho chuo ni wazembe mno!