Chuo Cha Mwalimu Nyerere-MNMA

Chuo Cha Mwalimu Nyerere-MNMA

mdaumzalendo1

Member
Joined
Feb 2, 2018
Posts
76
Reaction score
50
Nimetembea baadhi ya vyuo hapa Jijini na kutazama kwa ujumla mfumo wa elimu,miundo mbinu n.k.

Kwa ufupi leo napenda nizungumzie Chuo Cha Mwalimu Nyerere.Nianze kwa kuelezea Location Yake.Kimandahari chuo kipo nje ya mji but katikati ya mji.Chuo Kipo Kigamboni maraa baada ya kuvuka pantoniMwendo wa dakika kumi kutoka linakopaki pantoni.Upande huu wa mji zaidi ni makzi ya watu na hakuna pilika pilika za katikati ya mji.Kwa wakti huo huo ni rahisi kufika maeneno mengi ya mjini kati ndani ya muda mfupi.

Gharma za maisha kwa hapa chuuoni ni nafuu sana kwani hostel za ndani ni nafuu na za njee pia ni nafuu na gharama ya chakula,standard meal ni nafuu pia kiasi kwamba mwanafunzi anaweza kupa malazi,na chakula kwa mwezi mzima kwa gharama ya 150,000 tu kwa mwezi kutegemea na mtindo wake wa maisha. Ada ya chuo pia ni nafuu na wana mfumo rafiki sana wa ulipaji.

MNMA pia kinaweza kuwa chuo cha pekee kutokana na mandhari yake inayotazamana na Bahari ya hindi.Mandahari hii inawezesha mtu kusoma huku ukipata upepo mwanana wa bahari.Maktaba ya chuo pia ina view nzuri ya bahari pamoja na maghorofa ya Posta

Kwa upande wa walimu,wengi wana ushirikiano mzuri kwa wanafunzi na wanaojituma.Kiufupi walimu wengi wanafundisha kama walimu wa sekondari yaani wanakupa material za kutosha na kukfuatilila kwa karibu kuhakikisha unaenda nao sawa.
o hasa kutokana na idadi ya wanafunzi ukilinganisha na nafasi iliopo.Jitihada zinaendelea kuhakikisha kuwa miundo mbinu inaboreshwa ili kukidhi mahitaji

Kwa ufupi,ndani ya miaka 10 ijayo.Chuo hiki kama kikiendelea na kasi hii hii basi kitakuwa moja ya vyuo vinavyoheshimika katika Stadi za jamii.

Kama kuna mwenye maoni zaidi anaweza kuchangia uzi huu
 

Attachments

  • new3.jpg
    new3.jpg
    58.4 KB · Views: 193
Mfumo wa malipo ya ada ni rafiki kwa maana na nmna gan
 
Nimekumbuka tulivyokuwa tunakwenda kutumia uwanja wao, hapo kwenye mikorosho karibu na bahari kujisomea. Wakati mwingine walinzi wao wakicharuka wanatufukuza wanachuo ambao sio wa hapo Mwalimu Nyerere!!!
 
Hamna chuo pale. UVCCM wengi wale waliopora mabox ya kura kinondoni wanatoka hapo
 
Back
Top Bottom