Wale washauri nasaha, na wanasaikolojia wanaotoa huduma ya ushauri katika kituo cha MARINATHA mjini morogoro wameamua sasa kufungua chuo maalumu kwa ajili ya kufundisha mambo ya mapenzi kwa vijana na wanandoa.
Baadhi ya kozi zitakazofundushwa ni pamoja na
A. Kwa ajili ya wenye ndoa au walio kwenye mahusiano
1. Namna ya kutawala 'mapenzi' ukiwa katika masomo (jinsia zote)
3. Mwanaume bora kwa mpenzi wake (kwa ambao hawajaoa lakini wana wapenzi) (wanaume tu)
4. Mwanamke bora kwa mpenzi wake (kwa ambao hawajaolewa lakini wana wapenzi) (wanawake tu)
5. Mume bora kwa mkewe (wanaume tu)
6. Mke bora kwa mkewe (wanawake tu)
7. Namna ya 'kumhandle' mpenzi asiye mwaminifu (jinsia zote)
8. Namna ya kufanya unapohisi mwanandoa mwenzio sio mwaminifu (jinsia zote)
9. Vikolezo vya kumfanya mpenzi wako aamue kufunga ndoa na wewe (jinsia zote)
10. Vikolezo vya kunogesha tendo la ndoa/ngono. (wanaume peke yao na wanawake peke yao)
B. Kwa ajili ya walio 'single'
1. Sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati (kwa wanawake tu)
2. Sifa za mwanamke mwenye mapenzi ya dhati (kwa wanaume tu)
3. Namna ya kuishi ili uwe mwanaume bora kwa wanawake (kwa wanaume tu)
4. Namna ya kuishi ili uwe mwanamke bora kwa wanaume (wanawake tu)
5. Jinsi ya kumtongoza mwanamke (kwa wanaume tu)
6. Jinsi ya kumtongoza mwanaume (kwa wanawake tu)
7. Namna ya kufurahia maisha bila mpenzi
Kwa sasa wadau wa chuo wanakamilisha hatua za mwisho za usajili. Chuo ilikuwa kianze tangu mwaka 2010, lakini kulikuwa na mabishano makali juu ya kuruhusiwa wananfunzi, na pia mtaala wa kozi ya 'vikolezo vya kunogesha tendo la ndoa/ngono' uliwekewa ngumu na wizara ya utamaduni, hata hivyo tumefanikiwa kuwaelewesha na baada ya marekebisho kidogo ya kupunguza 'makali', mtaala umekubaliwa.
Baada ya siku chache watatoa matangazo kwenye magazeti na vipeperushi.
Vyote mnakaribishwa.