Habari za muda huu popote mlipo ndugu zangu.Mimi ni mwanafunzi muhitimu wa Chuo cha Madini Dodoma. Nimefanikiwa kumaliza chuo mwaka huu wa masomo 2016/2017.
Miezi miwili baada ya kumaliza masomo nikapokea ujumbe wa kuwa result statement ziko tayari, na kwa hivyo kwa yeyote alie tayari basi anaweza kuifata kwa wasaa wake.
Kwa mwenye njaa yoyote(mwenye kutafuta ajira) huo ndo utakuwa muda muafaka wa kutafuta tonge ya dhahabu(ajira) ambapo kwa kuanzia inabidi nifunge safari hadi Dodoma kufata result statement.
Nimefika Dodoma hii ni week ya pili inaenda bila kufanikiwa.Kikubwa unachoambiwa ni kuwa mara imepelekwa kwa registrar na siku zinazofuata humkuti kazini kabisa kwa kipindi chote cha wiki mbili(ingawaje hajasafiri).
Na kwa kuwakumbusha tu,ni wanafunzi watatu tu kwa muda wote huu wa wiki mbili ndo waliomba kupatiwa result statement.
Kipindi hiki ambacho vyuo vimefungwa mwanafunzi unakosa sehemu ya kujiegesha. Na kwa wastani wa nyumba ya kulala wageni ni tsh 15,000 kwa siku.
Ikiwa chuo chenye uwezo wa kudahili wanafunzi 300 tu kwa mwaka na wanafunzi watatu (3) tu walioomba result statement bado kinakuwa na ukakasi wa namna hii JE TUTAFIKA?
Lakini hayo yote ni tisa. makala ya JE TUTAFIKA ikakutana na jambo la kumi.Ambalo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Petroleum Geoscience pamoja na Geology and Mineral Exploration na wale kaka zao wa mwaka wa pili wa kozi ya Petroleum Geoscience hawakuenda kupata mafunzo kwa vitendo (Field) kwa sababu ya kuwa chuo hakina hadhina yoyote.
Ikiwa hizi ni moja ya core modules je watoto hawa watajumlishiwa vipi matokeo yao kamili ya GPA ikiwa uonevu tu.
Lakini swali jengine linakuja kuwa je hiki ndo kikosi halisi chini ya Wizara ya Nishati na Madini MEM tunachokiandaa kuja kushughulikia rasilimali za nchi hii.Na hapo ndo swali la msingi linapokuja:
JE TUTAFIKA?

Ahsante mkuu