Hawajui kuwa Watanzania bado tunautazama uongozi huu kwa jicho la tahadhari. Wapo wanaohoji sababu za teuzi nyingi kuangukia kanda moja, wapo wanaohoji uvunjaji wa misingi ya demokrasia, wapo wanaohoji kufinyangwa kwa mamlaka ya Bunge, n.k. Hatuwezi kufurahia utendaji mzuri katika jambo moja huku 10 yakiharibiwa.