Tatizo lenu washabiki wa Yanga huwa hamuamini kwamba timu yenu inaweza kupigwa ndani ya uwanja kwa kuzidiwa uwezo, mkifungwa mtaleta visingizio vya kila namna, mara wachezaji walijiamini, mara timu ilikuwa na mgogoro au wachezaji walipokea fedha au refa alihongwa. Kuna haja ya kuwa wanamichezo na kukubali kama timu imezidiwa na kufungwa kihalali kabisa.