G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,614
- 8,617
Najaribu kujifikilisha jambo.hapo zamani kabla ya mzungu na mwarabu kutuaminisha imani ambayo mababu zetu hawakuzijua.tuliamini tulichoamini bila jina Muhamad wala Yesu.na tulifanya mambo yote yatuhusuyo kwa imani zetu,vile vile tulikua na watu wenye nguvu na uwezo wa kiuungu kama kina Ngw'anamalundi huku uSukumani na wengine wengi.walitenda mambo makubwa kufanana na hao tulioletewa baadae kua ni mitume wa haki.sipingani na imani zingine ila najaribu kuwaza je?
1. Iwapo tukiamua kurudi zama zile kwa maana ya imani tutapatwa na baya lipi?
2. Iwapo tusipokili YESU na MUHAMAD kua ni wakombozi wa kweli tutaaminije kua kuwakataa kwetu tutaenda kuchomwa huo moto wa milele tunaohubiliwa?
3. Uchawi tuliokua nao ni kama sayansi ya leo na isiyoamini uchawi.iwapo tutaamua kuuboresha uchawi kua wenye tija na endelevu nini kibaya chaweza kutupata?
4. Tukiwasema kina Kinjekitile,mtemi Milambo,Mkwawa,Ngw'anamalundi ktk vitabu vyetu vipya tukimaanisha kama tusomavyo leo kina Yohana,Mathayo,Zakayo n.k
nini kibaya kitatokea kwetu katika maisha?
Ni hayo tu.