FUNDI CHEREHANI
KIJAKAZI WA KIUME
Sehemu Ya 61....(.19.)
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
"haaaaaaaaa"
"sasa utafanyeje sheby... Na akijua itakua msala, ila mi nimemwambia sijavaa chupi leo, ndio akakimbilia huko kwako"
"ok sawa nimekuelewa"
Nilikata simu afu nikaiweka mfukoni kisha pale pale nikaanza kutabasam kama vile namdanganyia kwa kumtabasamia,.... Lakini alikua kanuna kweli kweli,
"naomba utoke nataka kubadili nguo"
"kwani mi ni nani yako"
"hata kama lakini sio kila muda uone maungo yangu"
"sitoki sasa kama hutaki acha"
Alikaa kabisa kwenye kitanda huku akiniangalia, sasa nikaangalia pale nyuma ya mlango kuna boxer niliiweka kwenye msumali na asnati hajaiona,.. Nikavua ile suruali hata kama yupo afu nikaiwahisha kuichomeka pale kwenye msumali ambapo kuna boxer, kana kwamba akisema sina boxer naitoa ile suruali pamoja na boxer yake,....
"yaani hili swala lazima nikaseme kwa baba"
"nini tena asnati"
"yaani wote mumerudi hakuna alievaa nguo ya ndani hata mmoja, wewe umevaa suruali tu, na yeye kavaa sketi peke yake, sitaki maswali lazima niseme kwa baba, huezi kutuchanganya ndugu wawili kwa wewe mmoja tu... Tena hebu nipishe mimi"
ENDELEA........
Daa nilianza kua na wasiwasi juu ya swala hili na wakati mwanzo nililiona ni simpo tu lakini naona linakoelekea ni kubaya, yani kule nisipotaka ndio huku, lakini sikutaka hio taarifa ifike kwa mzee hivyo niliwahi kumzuia asnati asiende kusema, mana akisema tu ishakua msala tena ni msala wa mauaji mana nikiikumbuka ile bastola, mmmhhh mpaka naskia kizungu zungu juu ya jambo hilo,
"asnati, kwani kuna nini?"
"niachie"
Nilimvuta mpaka chumbani na kumlaza kitandani na wakati huo nilikua uchi kabisa, mana suruali niliivua muda huo huo,
"kwani shida nini asnati"
"sheby, nimekupa bikra yangu kwa mapenzi yangu, lakini why umeenda kutembea na mdogo wangu"
"aakhhhiii we nani kakuambia nimetembea na mdogo wako"
"yeye hana chupi, na wewe huna boxer, why kitu kama hiki na mumetoka wote njia moja"
Asnati alikua anaongea huku akilia tena kwa hasira mno,
"iv we Asnati unaakili kweli, mimi nisivae boxer nina matatizo gani"
Sasa kusema hivyo akapandwa na hasira iliomfanya aamke pale alipo na kuichukua ile suruali ili anionyeshe kua kwanini nimeivua bila boxer, Lakini alipoichukua aliikuta ikiwa na boxer ndani yake,... Kama unakumbuka niliiweka juu ya boxer
"mschiuuuuuuuu"
Alinisunya kwa kukutana na boxer ikiwa imeambatana na suruali yangu, alinitupia ile suruali kisha akaondoka kwa hasira zake,
Nami nikaendelea kulala kwa kuchoka mana sauna kanichosha kweli afu mbaya zaidi jumapili ya kesho mama Kelvin nae kaniahidi kunipa penzi, sasa sijui itakuaje Kwakweli, mana nimechoka kiasi kwamba sidhani kama nitaweza kumuhudumia mama huyu, ila nilipata wazo moja la kumkwepa kwa siku ya kesho, hapo hapo nikaanza kujifanya naumwa ili kesho asiwe na wazo la kuniita, unajua mama Kevin ni jimama haswa ila naona kama sintomueza kimapenzi mana sijawahi kutembea na jimama kubwa kama hili,
HATA MIMI MARA YA KWANZA NILIPOKUA NAANZA MAPENZI NILIKUA NI MUOGA SANA KIASI KWAMBA NIKIPANGA PROMISE NA MSICHANA, NAJIKUTA NAIPANGUA MIMI MWENYEWE KWA WASIWASI WANGU WA KUTOMFIKISHA KILELENI, JAMBO HILO LINAATHILI VIJANA WENGI AMBAO HAWAJAWAHI KUFANYA MAPENZI, HUA ANAWAZA SANA ILE SIKU YA KWANZA YA KUFANYA MAPENZI... NA KAMA UNA WASIWASI NA HILO, BASI TAFUTA MWANAMKE MSHAMBA MSHAMBA UANZE NAE, MANA DEMU MSHAMBA MSHAMBA HUSUSANI BEKI TATU WALE WA VIJIJINI KABISA AMBAE NDIO MARA YAKE YA KWANZA KUFANYA KAZI ZA NDANI, (HOUSE GIRL) AU YULE AMBAE HANA SWAGA ZA KISASA, WE MRUBUNI TU UTAKAVOJUA ILI UKAANZE NAE, UKISHAANZA TU BASI LAZIMA UE MZOEFU, LAKINI UKIANZA KWA DEMU CLASSIC, UTAKOMA KURINGA, ATAKUDHARAU MWANZO MWISHO MANA AMESHAPITIA WANAUME KABLA YAKO.... SASA MIMI SIJAWAHI KULALA NA JIMAMA, HUO NDIO WASIWASI WANGU, JAPO NILISHAWAHI KUMPONYA PONYA MARA KADHAAAA
Basi nilianza kua mgonjwa kuanzia siku hio ili kesho jumapili anikute naumwa, mana licha ya kumuogopa, lakini bado nimechoka kiasi kwamba sintoweza kufanya hivyo, au sintoweza kumridhisha kimapenzi,
Ilipofika usiku wa siku hio ya jumamosi walishangaa hawanioni sebureni kule, mana kuna muda ukifika wanaangalia movies alizoigiza dada yao, BATULI sasa hua wananiitaga niende nikamuone dada yao anavyofanya vizuri na akina ray, sasa siku hio niliku siriasi na ugonjwa japo sikua na ugonjwa wa ukweli ukweli,
Ghafla zakumu alikuja na kuniita
"wewe,..... sheby... Nyoo unajifanya umelala"
Nilikua kimya ili kuweka usiriasi wa ugonjwa
"jamani sheby, kwaio ndio unaninyamazia"
"we zakuu mi naumwa eti"
"heeeeeeee unaumwa? Unaumwa nini tena jamani baby"
Zakuu alikaa kitandani huku akinikagua kajoto flani hivi,
"limekuanza lini hilo homa"
"niliporudi twisheni tu kumchukua sauna ndio likaanza"
"wewe sasa kwanini usiseme tukakupeleka hospitalini"
"usijali nitapona tu"
Zaku aliniletea chakula huku huku chumbani kwangu japo hawapendi niwe nakula peke yangu huku, ila siku hio haikua na jinsi ya kufanya, siku hio ya jumamosi ilipita na leo ni jumapili mida ya saa 4 hivi asubuhi, nikiwa ndio kwanza hata kuamka najifanya siwezi na wakati huo nilikua nakula karanga na maziwa ili kuweka afya vyema, mana hii mitoto ya humu ndani kwa mitego tu haijambo, kama kawa mama Kevin alileta supu moja nzitoo huku akiipulizia na mdomo afu steki maini yote kaniekea na kalimau kwa mbali, sikuikopesha niliipiga huku mama Kevin akiwa kama ananionea huruma hivi kumbe walaa mtu wa watu ni mzima mpaka basi sema nimeumwa kwa ajili yake,
"pole"
"asante boss"
"jamani sheby, lakini kwanini usingesema toka jana,.... Ok lakini sio tabu ila hebu jiandae twende hospitali ukachekiwe afya yako"
"usijali mama Kevin, mimi najijua naponaje hivyo tusiharibu pesa"
"hapana lazima twende hospitali"
"please please mamy, sintokwenda huko nakuomba sana"
"yaani sheby ninavyokutamani, sipati picha itakuaje siku tukikutana"
"mbona unantisha mamy"
"hapana sikutishi, ila nakuambia tu, nakupenda sana sheby, siko tayari kukuona ukiwa huna raha ukiwa ndani ya himaya yangu... please please baby, naomba upone haraka sawa ee"
"usijali mamy nitapona tu kwa uwezo wa mungu"
Mama Kevin aliondoka zake, nami huku nyuma nikajisifu kwa ujanja wangu ulivyokwenda sawa kama nilivyotaka,
Leo ni siku nyingine ya juma tatu, nikiwa nipo njiani kuelekea shule, mana ile siku ya kuuana kimapenzi haipo tena, nilikua nawapelwka watoto wa boss shule, na kudai kua homa limepungua pungua, kumbe woga wangu ulikua ni ile siku ya jumapili tu,..... Saku ya leo Asnati alikua kanuna kweli kweli, ila nami nilimnunia kwa maana ya kwamba jana kanisunya kaniona fara, sasa na mimi leo nakaza butu staki mazoea na yeye mpaka aniombe masamaha... Niliokua naongea nae kwenye gari alikua ni sauna tu peke yake ila Asnati yeye kanuna ile mbaya,
Niliwafikisha shuleni kisha nami nikarudi nyumbani kwa kumchukua mzee nae ili nimpeleke kazini, nilipofika nyumbani nilimkuta mzee katulia zake sofani akinisubiria...
"shkamoo mzee"
"marahaba kijana ujambo?"
"sijambo, sasa mzee si tunaenda sasa"
"ndio tunaondoka ila leo kuna mahali tupitie mara moja"
"hakuna shida mzee"
"ilaaaa una suti"
"suti??"
"ndio i mean nguo za suti"
"aaahh hapana mzee sina"
"ok basi haina shida tutanunua huko mbele"
Sasa nikaanza kujiuliza kwanini mzee kaulizia suti, sasa anataka niwe na suti ili iweje, nilikua sipati majibu juu ya jambo hilo,.... Niliwasha gari kisha tukaondoka kuelekea kazini, lakini yeye kasema kuna mahali nimpitishe kwanza, sasa nilishangaa akiniambia tuingie katika duka moja lenye nguo za heshma, hususani suti,...
"haya chagua itakayokupendeza hapo"
Kiukweli sikua na maswali ya kumuuliza bali nilianza kuchagua suti kali kali nikapata moja nyeusi, kisha mzee akalipia gharama ya suti hio, yapata kama laki 6 hivi,... Kama ni mimi binafsi nisingenunua,
"tafuta mahali uivae tunachelewa"
Daaahh niliingizwa kwenye chumba kimoja kidogo hivi cha kubadirishia nguo, Niliingia na kuanza kubadiri nguo,
Lakini ghafla nilianza kusikia sauti ndani ya chumba hicho, ila ilikua ikijirudia rudia mara kwa mara kama vile ndani ya daraja
"Una bahati ya pekee, pekee, pekee, pekee, na utakachokabidhiwa we kipokee pokee pokeee, pokee... Lakini chaweza kua kilio ndani ya familia yako, yako, yako, Yako"
Nilishtuka sana kwa sauti hio na sijui ilikua inaniambia mimi au? Nilijikuta nimevaa suti hio bila hata ya kuvaa tai kutokana na wasiwasi niliokua nao,
"vp mbona hujafunga tai sasa"
"aaahh mzee siwezi kuifunga tai"
Nilidanganya kua siwezi lakini sio kua siwezi sema kile kilichoongea kule ndicho kilichonishtua mapigo ya moyo,.. Basi mzee alinicheka kwakua sikua najua kufunga tai, hivyo akawa ananifunga yeye, tulipomaliza, tulipanda gari na kuondoka, na wakati huo nduo zangu zile nimeacha kule kule kwanye kile chumba, niliwasha gari mpaka hapo tulipotakiwa kufika, tulikuta magari mengi sana ya kifahari, yaani magari ya kuanzia milioni 100 kwenda mbele, tulipaki vx yetu kisha tukaingia ndani, yani hilo jengo lenyewe ni kali humo ndani usipime, nakumbuka limeandikwa TRCC ( Tanzania Rich's Conference Center) Yaani hio ni Sehemu ya mikutano ya matajiri wote wa Tanzania, Niliingia huku nikiogopa ogopa, Tukapanda lift ya kuelekea ghorofa ya juu, tulipofika tulikuta watu wengi sana, ila kitu kilichonipa moyo ni kwamba kulikuepo na vijana lika langu, hapo ndipo kidoogo nikawa na amani mana kuna vijana wenzangu wengi sana, Yaani kulikua na siti mbili tu, kama vile tulikua tukisubiriwa sisi,.... Sikua najua kinachoendelea kwani hata watu tuliowakuta walikua kimyaa, afu mbele kuna kama jukwaa hivi kwa ajili ya mtu ambae atakua akiongea nasi tunamuangalia, walianza kwenda mbele kwa foleni, yaani mtoto anenda na baba yake pale mbele kisha anamuachia nyalaka za makampuni atie saini mbele ya matajiri wengine,.. Sasa hapo ndipo nilipojua kua huyu mzee kanileta huku kama mtoto wake, na huenda akanikabidhi mali zake kama wanavofanya hawa wazee wengine,.... Walifatia wengi sana na hatmae ikafika zamu yangu au zamu ya mzee Yusuf, Mzee alinishika mkono huku tukielekea katika kile kijukwaa kule mbele, mzee akaanza kujitambulisha yeye kama yeye,
"leo ni siku nzuri kwenu na hata kwangu pia, na nina furaha sana kwakua ninae mrithi wa mali zangu"
Papo hapo mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio kwa kusikia maneno hayo,
"huyu ndio mtoto wangu ninaemtegemea katika hili, huyu ndio tajiri anaefuata madala yangu,... Kwa jina naitwa Yusuf Barati Husein nina kampuni sita na sheli mbili za mafuta na kiwanda kimoja cha unga, na mali zoote hizo atamiliki mtoto wangu huyu hapa, na nyalaka za mali hizo hizi hapa na namkabidhi atie saini mbele yenu"
Mzee huyu aliweka makaratasi mezani kisha akamuita mwanasheria aliopo mbele yetu, kwa ajili ya kuhakiki mikataba hio au hati miliki hizo... Mwanasheria alizikagua na kusema kua
"hati miliki za bwana Yusuf barati husein ni sahihi kabisa, ila imekosekana saini ya mtoto wake"
Mwanasheria alinigeukia mimi na kuniambia
"kijana, tunaomba ujitambulishe kisha usaini mikataba ya baba yako kua yako"
Wakati huo mzee mwenyewe kesharudi kukaa, hivyo hapo natia saini mwenyewe nikiwa kama mtoto wa huyo mzee,...
Sasa nikiwa naisoma ile mikataba ya makampuni 6 na sheli mbili na kiwanda kimoja cha unga... Niliskia tena zile sauti zikisema,
"fanya haraka kwani una watu wawili wa kukusainisha mali zao"
Nikashikwa na mshangao watu wawili kivipi, na huyo wa pili ni nani...
Mara mwanasheria akaniambia
"kijana tunakusubiri wewe"
Nikamaliza kusoma kisha nikawageukia matajiri wenzangu, mana tayari nishakua tajiri, hivyo nikaanza kupungia mkono
"namshukuru sana baba yangu kwani hakua na familia nyingi tofauti na yetu"
Watu walishangilia na kumpa sifa mzee Yusuf, kua hakua mtu wa michepuko
"kwa sasa nina furaha juu ya jambo..... "
Sasa ghafla nikashikwa na butwaa baada ya kuona kiti kimoja ambacho kilikaliwa na mtu mmoja ambae sikutegemea kama angalikuepo huku.....
"kijana vp? Unachelewa, watu wengi sana wa kusainisha watoto wao"
Hio ni sauti ya mwanasheria akiendelea kunikazia buti....
Sasa kuanzia hapo nikawaza kubadiri jina ili huyo mtu asinijue kama ndio mimi alionidhania.... Na nisipo badirisha jina basi ile kauli iliosema kua
(nasubiriwa na watu wawili wa kunisainisha mali zao) Itatimia, hivyo kubadili jina ni lazima japo itakua mbaya..
Je? Nitajiita jina gani... Na je huyo mtu ni nani?....
USIKOSE KUIFATILI SEHEMU IJAYO KESHOKUTWA
Itaendelea..... after Tomorrow
KWA SIMULIZI ZAIDI BOFYA HAPO CHINI, KISHA UNGANA NASI KWA KUGONGA LIKE KWA HIO PAGE YETU →→→↓↓↓
Chombezo Media | Facebook
USIKOSE HAPO KESHOKUTWA USIKU... MIDA KAMA HIII HAPA