China yasema inahofia vitisho vya nyuklia vya Korea Kaskazini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
_95703623_mediaitem95703620.jpg


China imesema kuwa ina waswasi mkubwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ,kufuatia mahojiano ya afisa mmoja wa taifa hilo na BBC.

Naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini aliambia BBC kwamba Pyongyang itaendelea kuyafanyia majaribio makombora yake na itarusha bomu la nuklia ikibaini kwamba Marekani inataka kuishambulia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lu Kang amesema kuwa China ilipinga vitendo ama matamshi ambayo huenda yakasababisha hali zaidi ya wasiwasi.

Kumekuwa na matamshi ya chuki kutoka kwa pande zote mbili katika siku za hivi karibuni.

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ambaye amekuwa akitembelea eneo hilo ameonya Korea Kaskazini kutoijaribu Marekani na kusema kuwa wakati wa subira dhidi ya Pyongyang umekwisha.

Mwandishi wa BBC Stephen McDonnel mjini Beijing anasema kuwa serikali ya China inaonekana kukerwa na Korea Kaskazini ambaye mwandani wake.

''Nimeona ripoti ya hivi karibuni," Bw Lu alisema kuhusu mahojiano hayo ya BBC.

''China ina wasiwasi mkubwa kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini na utengenezaji wa silaha''.

China inaunga mkono mpango wote wa kusitisha uundaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea, kuimarisha amani na uthabiti katika rais ya Korea mbali na kuendelea kutatua maswala tofauti kupitia mazungumzo na majadiliano.

Korea Kaskazini ilifanya maonyesho ya gwaride la kijeshi wikendi iliopita na kujaribu kombora jingine siku ya Jumapili ambalo Pentagon inasema lililipuka muda tu liliporushwa.

Pyongyang imesema kuwa itafanyia majaribio makombora yake kila wiki na kuonya vita vikubwa iwapo Marekani itaishambulia.

_88837990_north_korea_missile_ranges2_map624new.jpg

Iwapo Marekani inapanga shambulio la kijeshi dhidi yetu,tutalipiza kwa shambulio la kinyuklia kwa kutumia mbinu yetu, alisema naibu wa waziri wa maswala ya kigeni Song-ryol siku ya Jumatatu.

Baadaye bwana Pence aliapa kulishinda shambulio lolote na kukabiliana na utumizi wowote wa silaha za kisasa ambapo zile za nyuklia kwa kujibu na shambulio kubwa.

Meli ya wanamaji wa marekani ya Carl Vinson inayobeba ndege za kijeshi pamoja na meli za kijeshi, inaelekea katika bahari ya magharibi mwa Pasifiki kulingana na kamanda wa eneo hilo kufuatia agizo la rais donald Trump wiki iliopita.

Imebainika kwamba wakati agizo hilo lilipotolewa meli hiyo ilikuwa ikielekea upande tofauti.

Haijulikani iwapo hatua hiyo ilifanywa kimakusudi, ni mabadiliko ya kimkakati ama mawasiliano mabaya kulingana na mwandishi wa BBC nchini Korea Stephens Evans.

Chanzo: BBC Swahili
 
kwa nyuklia aliokua nayo huyu mapanki wala hahitaji missile kuzirusha, akiziripua pale kwake tu basi hata china nae ataisoma namba. south korea yote itakua jangwa. ni vyema wakatumia diplomasia kusuluhisha huu mgogoro
 
By the way China ni rahisi kushawishika na NATO kwA Hyo Dogo amalzie tonge LA mwisho akampe hai Sadam na scud zake. Watakacho fanya US, NATO, Israel, Japan, China na nyinginezo kwA Kua wamejua anacho ringia watamuwah kulipuaa na ku haribu NUKS za NK vinu vyote then Dogo atachapwa kipigo cha mbwa mwizi. China hawezi kukubali mzozo uishe bila NK kusitisha Utengenezaji wa Nuks Kwan anaogopa kipindi US akiachana nao China hawez kumpiga
 
Nilikuwa najaribu kuangalia air distance hapa; nimegundua Pyongyang is closer to Dar-es -Salaam than to Washington DC.

Pyongyang - Dar-es-Salaam: 10198.24km
Pyongyang - Washington DC: 11054.01km

Endeleeni kumshabikia mwendawazimu mkidhani mko salama.
 
Inasikitisha kuona mnao shabikia hii vita itokee,najua hamjui madhara ya vita..nilipoteza wazazi na baadhi ya ndugu ktk mauaji ya kimbali.
Waoneeni huruma wakorea na wamarekani wasio na hatia vita haina macho ndugu zangu inaacha makovu yasiyofutika
 
Inasikitisha kuona mnao shabikia hii vita itokee,najua hamjui madhara ya vita..nilipoteza wazazi na baadhi ya ndugu ktk mauaji ya kimbali.
Waoneeni huruma wakorea na wamarekani wasio na hatia vita haina macho ndugu zangu inaacha makovu yasiyofutika
 
Back
Top Bottom