Pilipilihoho
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 202
- 145
Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na rais Joachim Gauck wa Ujerumani hapa Beijing, na kukubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano wa kiwenzi wa kimkakati kati ya nchi zao kwa pande mbalimbali na pia kuongeza ushirikiano katika kukabiliana na changamoto duniani.
Rais Xi amesema China na Ujerumani zinashuhudia mawasiliano na ushirikiano mzuri zaidi kuliko siku zilizopita na uhusiano wa pande hizo mbili unaelekea kwenye ngazi ya juu. Amesisitiza kuwa nchi hizo mbili zinatakiwa kuheshimiana, kutendeana kwa haki na kuzingatia maslahi makuu ya upande mwengine na kuimarisha uaminifu wa kisiasa.
Naye rais Gauck amepongeza kazi za kiujenzi zinazofanywa na China katika masuala ya kimataifa, na kusifu uwazi na athari nzuri ya pendekezo la "Ukanda mmoja na Njia moja". Amesema Ujerumani inapenda kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na China na kukuza ushirikiano kati ya Ulaya na China.