Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Waziri mambo ya nje China kufanya ziara Tanzania Januari 09, 2017 atajadili mpango wa uendelezaji wa viwanda ambapo China itajenga viwanda 200 kabla 2020.
Mbali na hayo ziara ya waziri mambo ya nje wa China nchini pia italenga kujadili miradi kadha wakadha ya maendeleo kama ifuatavyo;
1. Maboresho reli ya TAZARA
2. Ujenzi bandari ya Bagamoyo
3. Ujenzi reli ya kati
Hayo yalibainishwa jana na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi.
Waziri Yi anatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi ijayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara hiyo, Mindi Kasiga, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa ziara hiyo imelenga kukuza uhusiano kati ya China na Tanzania na kuangalia maeneo mapya ya kiuchumi.
Alisema viwanda vitakavyoanzishwa na Wachina nchini vitagusa maeneo yote muhimu ikiwamo sekta ya kilimo.