Chimbuko la ubatizo wa maji mengi

Chimbuko la ubatizo wa maji mengi

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
110
Reaction score
210
Chimbuko la ubatizo wa maji mengi

Yesu alisema hivi: "Amini, Amin, nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu" (Yohana 3:5). Kuhusu ubatizo, ni muhimu kufahamu kuwa Yohana mbatizaji alimbatiza Yesu katika maji tele (Mathayo 3:13-17). Yesu Kristo alibatizwa katika mto Yordani kwa sababu huko kulikuwa na maji tele.

Chimbuko la ubatizo wa maji mengi


(i) UBATIZO kwa lugha ya Kiingereza, ‘baptism’, maana yake Kiebrania ni "kuzamisha kabisa chini ya". Hivyo, ubatizo wa maji mengi maana yake ni kuzamisha kabisa chini ya maji. Ndilo chimbuko la ubatizo wa maji mengi.

Tafsiri yake ilikuwa ni aina ya kufa, kuzikwa na kufufuka kwa Kristo (Warumi 6:3-5). Hivyo, unapozamishwa majini, tafsiri yake ni kuwa unakufa na Yesu na kufufuka na Yesu. Maana yake ni kwamba ya kale yamepita, tazama, umekuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo.

(ii) Ubatizo wa maji mengi unadhihirisha kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Yesu mwenyewe alipobatizwa kwa maji mengi (mto Yordani), alidhihirisha kile ambacho alikuwa amekwenda kukifanya ili kutukomboa.
Ubatizo wa maji mengi hautuokoi ama kuchangia cho chote katika ukombozi wetu, bali ni udhihirisho wa kuwa tumeokolewa.
Ubatizo wa maji mengi ni kielelezo kikubwa ya kwamba mtu amempa Yesu moyo wake na maisha yake.

(iii) Ubatizo wa maji mengi unadhihirisha kufa kwa maisha ya kale/zamani yaliyokuwa mabaya mbele za Mungu, na kuzikwa kabisa, na sisi kufufuliwa katika maisha mapya ndani ya Yesu Kristo.

Hiyo ndiyo sababu ya kuzamisha wakati wa ubatizo wa maji mengi. Ni kudhihirisha mtu wa zamani kuzikwa, na mtu mpya kufufuliwa katika uzima mpya.

Kitabu cha Warumi 6:4 kimesema:
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima".

Yohana mbatizaji alikuwa akibatiza sehemu zenye maji tele ili watu waweze kuzamishwa katika maji
. Yohana mbatizaji hakubatiza Yordani tu, alibatiza Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Yohana 3:23: “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele, watu wakamwendea wakabatizwa”. Ubatizo lazima ufanye kwenye maji tele ya kumtosha mtu kuzamishwa.

Matumizi ya maji kidogo kwa ubatizo, kama ilivyoainishwa kwenye Matendo 2:41, Matendo 16:15 na Matendo 16:33, yalikuwa ni katika mazingira maalum ya papo kwa papo tu, pamoja na mazingira ya mgonjwa mahututi, nk. Matumizi ya maji kidogo haistahili kuwa njia rasmi ya ubatizo, kwani hakuna uhaba wa maji mengi ya kubatizia, hususan kwa ajili ya visima vidogo tu vinavyohitajika kwa shughuli hiyo.
Kulingana na maandiko, kama ilivyoelezwa hapo juu, matumizi ya maji mengi ndiyo njia rasmi ya kubatiza.
UBATIZO WA MAJI MENGI ULIANZISHWA NA YESU MWENYEWE KATIKA MTO YORDANI. HIVYO, MABISHASHANO HAYATARAJIWI KUWEPO KUHUSU JAMBO HILO, KWANI HAKUNA MAHALI ALIPOTENGUA JAMBO HILO, BADALA YAKE ALILIKAZIA KUPITIA
MATHAYO 3:13-17; MARKO 1:9-11; LUKA 3:21-22, sawia:

“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.
Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?
Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote.
Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha batizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye”.
 
Back
Top Bottom