Wapendwa wanajamii,
Kama ambavyo tunamsoma chifu Mangumgo kwenye historia ya Tanganyika na yale aliyoyafanya,
"NAPENDEKEZA TUWE NA ORODHA YA MAJINA YA WAHUJUMU UCHUMI WANAOUZA NCHI YETU LEO KWENYE HISTORIA YA TANZANIA".
Yaorodheshwe majina yao, yaainishwe madhila ya kila mmoja wao na vizazi vyao, watoto wetu wafundishwe kwenye historia. Aibu hiyo itawafanya viongozi wa kitaifa kufanya kazi kwa manufaa ya nchi. Historia hiyo isifungwe na yeyote atakayejiingiza sasa na baadaye kwenye MATENDO HAYO AINGIZWE kwenye orodha.
Tunayo mengi ya kuandika na mengine yameandikwa humu kuhusu individuals wanaojihusisha na ufisadi unaodidimiza taifa. Tusicheke na nyani, tutavuna mabua.
Nawasilisha