Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,149
- 43,096
Uhamisho wa mshambuliaji Armando Broja kwenda Burnley unamaanisha kuwa klabu ya Chelsea imefanya mauzo zaidi ya Pauni milioni 250 kwa wachezaji kutoka akademi yao ndani ya miaka mitatu pekee.
Todd Boehly na Clearlake Capital, wakisukumwa na shinikizo la kanuni za faida na uendelevu za Ligi ya Premia (PSR), wameharakisha mkakati ulioanza chini ya mtangulizi wao kama mmiliki, Roman Abramovich. Katika hali hii, kuondoka kwa Broja kwenda Burnley kuna thamani ya hadi pauni milioni 20 ikiwa nyongeza zote zitatimizwa, na hivyo kufanya jumla ya uwezekano wa mauzo ya wachezaji wa Akademia yao msimu huu kufika pauni milioni 41.2.
Cha kufurahisha kwa Uongozi wa Chelsea ni kuwa wachezaji wa Akademi wanahesabiwa kama Faida katika hesabu za klabu, kuondoka kwao kumeipatia Chelsea uwezo wa kukua kifedha - na kusaidia kukusanya pauni milioni 250 huku ada za uhamisho zikipunguzwa kwa kusaini Kandarasi za muda mrefu na kulipa kwa awamu.
Burnley pekee wamechangia zaidi ya pauni milioni 55 kwa Chelsea kupitia manunuzi ya wachezaji majira haya ya Joto, wakiwasajili Kiungo wa Kati Lesley Ugochukwu na mshambuliaji Armando Broja kwa ada zinazoaminika kuwa zaidi ya pauni milioni 20 kila mmoja licha ya kutokuwekwa wazi (undisclosed fee).
Ukiweka mauzo ya Noni Madueke na Djordje Petrovic yameongeza kiwango cha mapato kwa Chelsea, huku klabu hiyo ikitarajiwa kuvuka mauzo ya pauni milioni 300 kwa wachezaji wanaoingia msimu huu na wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili Alejandro Garnacho wa Manchester United huku Xavi Simons wa RB Leipzig akisalia kulengwa kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama mnamo Septemba 1.
Msione wanatumia sana Pesa wana namna yao ya kuzirudisha.😅