Chanzo cha CORONA - COVID 19

Chanzo cha CORONA - COVID 19

mitindo huru

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2016
Posts
1,610
Reaction score
1,601
Hadi leo mataifa makubwa mawili katika hii sayari dunia, taifa la China na Marekani wamekua katika mzozo mkubwa kuhusu nani alieanzisha ugonjwa wa COVID 19.

Madai ya China ni kwamba Marekani ndio aliyeanzisha ugonjwa wa COVID 19,
China inadai kwamba Marekani ilitumia wanajeshi wake walioenda China kwa mafunzo ya pamoja mwaka jana na ndio muda huo wanajeshi wa Marekani walipeleka virus hivyo nchini China

Madai ya Marekani kuhusu China kutengeneza virus hivyo ni kwamba, wanasayansi wa China walitengeneza virus hivyo maabara na badae wakashindwa kuvidhibiti hadi kupelekea kusambaa jijini Wuhan nchini China na kisha dunia nzima.

Madai ya Marekani yanaonekana kupata nguvu zaidi sababu ugonjwa huo ulianzia nchini China na pia China imeonekana kudhibiti ugonjwa mapema kuliko mataifa mengine hali inayoonekana ni kama taifa lililojiandaa na huu ugonjwa.

Pia inasemekana mataifa haya yanashutumiana kwa sababu za kiuchumi ,

Wapo wanaosema China kaanzisha huu ugonjwa ili aweze kuwa juu kiuchumi duniani kwa kudhoofisha nchi zingine kiuchumi hasa Marekani na Ulaya ambao ndio washindani wake wakubwa kiuchumi.

Pia wapo wanaosema kwamba Marekani kaanzisha huu ugonjwa ili aweze kudhoofisha uchumi wa China kwa kumuongezea maadui kwa nchi ambazo China ni washirika wake wakubwa mfn Iran, Russia, Afrika n.k

Pia kuna madai mengi kutokana na nchi husika mfano Waarabu wanamadai yao sababu ugonjwa huu umevuruga biashara ya mafuta duniani ikizingatiwa nchi nyingi za kiarabu zinatumia nishati ya mafuta kama ndio chanzo chao kikuu cha mapato.

Pia watu wa dini hasa Ukristo, uislamu, Hindu n.k wanamadai yao sababu ugonjwa huu umevuruga utaratibu wa ibada kwenye maeneo yao yaliyozoeleka kufanya ibada n.k wao wakisema ugonjwa huo umeanzishwa ili watu wasiweze kuabudu Mwenyezi Mungu kwa kufanya lockdown.
Hivyo ni kama wanalazimishwa kutoabudu katika maeneo yao yaliyozoeleka ili kumpa nguvu shetani ya kutawala watu.

Wengine wanadai ugonjwa huu unasababishwa na technology ya mawasiliano ya mtandao yani 5G wakisema kwamba hiyo technology ndio inasababisha watu waweze kupata dalili kama mafua kali, homa kali, kikohozi Kikali, kukosa pumzi n.k na mwisho kufariki
Kwenye haya madai wakaenda mbali zaidi na kusema hiyo technology ya 5G inaanzishwa ili kuweza kusaidia mfumo wa artificial intelligence kufanya kazi vizuri, sababu wanadai mfumo huo wa artificial intelligence unahitaji mtandao wenye nguvu sana wakaona 5G ndio jibu la mipango yao.

Wakaendelea na kusema katika hiyo artificial intelligence kuna mfumo wa Microchip utaowekwa kwenye mwili wa binadamu kwa kutumia chanjo ya COVID 19, hivyo watatumua COVID 19 kama sababu feki ya kuwalazimisha watu chanjo.

Pia wakidai lengo la hiyo Microchip ni kuweza kumsimamia binadamu asilimia kubwa ya mambo anayofanya kwa kutumia hiyo Microchip itakayowekwa mwilini mwa binadamu,
wakiongezea zaidi kwa kusema ndio maandalizi ya utawala wa Shetani kwa kutumia serikali moja ya dunia yani New World Order.
Hivyo ambao watakataa hiyo chanjo yenye Microchip inawezekana watakatazwa kufanya mambo mengi ya Kijamii mfano kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine, kupata huduma muhimu n.k

Hivyo hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya kwamba nini chanzo cha huu ugonjwa na pia hatujui agenda zilizopo nyuma ya huu ugonjwa

Wito wangu kwa watanzania ni kuacha kufata kila kitu kinachofanywa au kusemwa na wazungu au watu Asia kuhusu huu ugonjwa sababu hatujui hasa nini kilichopo nyuma ya huu ugonjwa na agenda zake za siri na pia hadi sasa hatumjui adui yetu.
Pia tujikumbushe kidogo kwamba hawa wazungu ndio waliotuletea magonjwa kama Ebola, Ukimwi, Homa ya Bonde la Ufa, Mafua ya ndege n.k

Mataifa makubwa duniani yanatumia nguvu kubwa kusambaza propaganda kuhusu huu ugonjwa na sababu wao ndio wanamiliki vyombo vyote vikubwa vya habari duniani kama BBC, CNN, ALJAZEERA, DW n.k hivyo inakua rahisi kwao kusambaza taarifa hata kama taarifa hiyo ina lengo baya kuhusu Afrika na dunia .

Hivyo pia ni vizuri Afrika hasa Tanzania, tukachunguza sana kwa uwezo wetu wote kuhusu chanzo na ajenda za siri zilizopo katika huu ugonjwa ili tujue hasa adui yetu ni nani sababu hadi sasa hatujui hasa adui yetu.
Pili ni vizuri katika kupambana na huu ugonjwa turudi katika asili yetu katika kupambana na majanga, hapa nasisitiza tukiona mwafrika mwenzetu kaonesha njia ya asili tusimbeze wala kumpuuza kwa kulinganisha na njia za wazungu kwamba njia za wazungu ndio bora kama nilivyosema awali hatujui adui yetu kuhusu huu ugonjwa.

Tumeona nchi kama Madagascar wanasema wanatiba ya huu ugonjwa, hivyo kama ni kweli ni vizuri tuitumie hiyo dawa na tuikuze hii taarifa dunia nzima katika forum zote duniani ili itambulike kabla adui tusiemfaham akavuruga.
Kuna watu wengi wapo Africa ikiwemo Tanzania watu hao wapo wataalam wa afya, waandishi wa habari, kampuni, NGO, wanasiasa n.k wanatumiwa na mataifa makubwa kusambaza propaganda ovu zikiwa na lengo la kukebehi, kudharau, na kupotosha juhudi mbalimbali za kweli zinazofanywa na viongozi wa Afrika katika kupambana na ugonjwa huo pia hata nchi za Afrika zikijaribu kujikomboa na mambo mbalimbali kama Kijamii, kiuchumi, kisiasa n.k
 
Nimesikitushwa kuona uzi mzuri kama huu ukikosa wachangiaji. Hongera sana mkuu, umewaza kwa kiwango cha juu sana.
 
Msimuliaji anasema corona ilitoka kuzimu na baada ya kuzimu kupigwa kombora moja zito sana na watu wengi sana walikufa kuzimu so wakaamua kuleta corona kupitia daktari wa kichina ambae ni agent namba *** yule daktari baada ya kuleta tu corona china katika jimbo la wuhan akarudi kuzimu. Lengo kuu ni Ili kuleta watu wengi sana kuzimu tena kwa mda mfupi Sana Ili kujaza lile gap la waliokufa kuzimu kwa mda mfupi Sana. Anasema baada ya kuzimu kujaza lile gap corona haipo imeisha. Huu ushuhuda nauunganisha na pindi magufuli aliwaambia watz waombe pia aligomea lockdown,corona itakwisha, pia wapo watu wa dini nao waliungana na Magufuli. Pia kazungumzia ishu ya chanjo na nini ajenda yake na ile chanjo inakwenda badili nini kuhusu ubinanadamu mbeleni.
Pia amezungumza kuhusu babu wa loliondo kwamba wao ndio waliomtengeneza hakuwa freemason but wao kama freemason walimtumia kwa kupitia nyota yake.
Mimi msimamo wangu hata kabla ya shuhuda hizi. Sichanji na sitochanja kwa maana nazijua siri za dunia na nani wapo nyuma ya ajenda hizi.


Babu wa loliondo

Jinsi wanavyotengeneza magonjwa

Sipendagi sana mambo ya unabii na utabiri wa siku hizi, lakini kwa kuwa unahusu corona nauunga mkono hata kama si kwa mtazamo huu. Kuna agenda ya siri juu ya corona. Haiwezekani wazungu wakulazimishe/ wakupe chanjo na pesa juu. Na kulazimisha nchi zote ziwachanje wananchi wao bure tu!!?. Naungana na wasiochanja wote duniani maana kuchanja ni hiari tusilazimishwe.
 
Watu wanataka kuchangia kula kimasihara lkn ikija mambo vyeti kimya
 
Back
Top Bottom