Changia mada: Malezi bora ya mtoto Tanzanian context

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Wadau hebu tupeane mawazo juu ya malezi bora ya mtoto ktk jamii za Kitanzania kwa sasa!

Najua kuna watu wenye taaluma zao kama Madaktari wa watoto, wana saikolojia, walimu na wataalam wengine wa elimu ktk Nyanja hii muhimu wanaweza kutupa maoni yao!

Nianze kwa kusema, malezi yamekuwa magumu sana ktk jamii yetu kwa sasa. Kuna nafasi finyu sana ya kupata mtu wa kuwasaidia wana ndoa wapya wanaopanga kupata mtoto (kama mimba haijatunga kwa bahati mbaya). Maandalizi ya wazazi pia hayaanzii ktk kupata partner, kushika ujauzito, kutunza mimba na kisha kumlea mtoto ktk vipindi tofauti hadi anapokuwa mkubwa!

Hebu tuone juu ya kumpata mzazi mwenzio
Wengi wetu huwa tunavutiwa na sifa za urembo na mafanikio ya kiuchumi kwa mwenza tunayemtafuta,which is good in a way lakini hatuwezi kuishia hapo tu. Mtu anayetarajiwa kuwa mzazi lazima achunguze na sifa nyingine za baba au mama wa mtoto wake, kumbuka partner wako leo ndiye mzazi wa mwanao kesho! Pamoja na sifa za uzuri(beautiful/handsome) lkn pia anatakiwa awe caring na responsible!

Wapo wazazi wanashinda bar na michepuko wakispend hadi 1 million kwa siku huku wakishindwa kulipa ada ya mil 1 kwa mwaka kwa ajili ya watoto wao! Wapo wanaozalisha watu na kukimbia familia! Pia wapo wadada wanaoshinda club na kuacha watoto kwa jirani au wakawaacha vijijini kwa bibi zao nao wakabaki kula bata mjini! Lkn wapo pia wanaokataa mimba na wenye kutupa watoto! So partner wako anapaswa achaguliwe kwa uangalifu maana yote haya yanaathiri malezi ya watoto!

Pamoja na sifa za mtu mmoja mmoja kama mwenzi, kujua aina ya familia anayotoka pia ni muhimu mno, unaweza kusema kuwa wazazi au jamaa wa mwenza wako hawakuhusu, nadhani ni big mistake, wanao wataenda kumuona babu, na kama kina uncles na aunts ni drug dealers unaweza ukajuta, ni sawa tu na kuoa au kuoelewa na mtu toka familia tajiri, kuwa kuna some advantages utapata japo kwa kutumia jina (eg ukoo wa kikwete, Magufuli, Mengi, Lowasa, Kaseja etc)

Vivyo hivyo kama utaingia ktk familia zenye majina mabaya wanao pia wanaweza kuwa levelled na kuathiri malezi yao! Kuna wagonjwa ya kurithi ndani ya familia, lkn kuna migongano ya kijamii ktk familia, avoid sana familia zisizokuwa na mshikamano,mifarakano na ugomvi wa kila mara hupunguza mapenzi ktk jamii hiyo pia kumfanya mwenza anayeishi ktk misukosuko akose furaha, awe mkali na mwenye hasira muda mwingi hivyo kukuathiri wewe na watoto wako, hivyo kuhatarisha suala zima la malezi bora ya mtoto!

Hebu tutazame mipango ya mimba na kuzaa!
Katika eneo hili wengi wetu mimba huzuka tu, wala hatupangi, lkn ukweli ni kuwa mimba huandaliwa, hata kama hujui lini utaipata Ila lazima mtu utambue kuwa sasa nipo tayari kuzaa! Ukifika muda wa kusema sasa nipo huru, mwanamke anapaswa aanze kwa kuitazama lishe yake, maana lishe bora ya Mama ni andalio zuri kwa mtoto anayetarajiwa!

Ni sawa na mkulima kabla hata ya kulima huwa anaandaa shamba na udongo wenye rutuba ni chachu ya kupata mazao bora! Shida kwa sasa wanawake wanajitahidi kujenga sex figures na wana starve ili wapendeze, please linda afya yako lkn usijinyime mlo, kuna virutubisho muhimu ambavyo mtoto atahitaji ktk wiki za mwanzo wa mimba muda ambao hata wengine wengi hawajui kama wajawazito!

Kuna mtaalam anasema madini kama folic acid yakikosekana ktk wiki 4 za mwanzo za ujauzito huweza kuleta matatizo mengi ktk ukuaji wa mtoto hasa magonjwa ya mfumo wa fahamu kama kuzaliwa na kichwakichwa kikilichojaa maji na mgongo wazi! So wamama wajitahidi kuhakikisha wanapata balanced diet! Ila pia hata wanaokula kupita kiasi na kujieletea uhatarishi wa obesity na wengine magonjwa ya mishipa ya damu kama pressure na pia shida kama kisukari matatizo haya kama yakimpata Mama basi kuna uwezekano wa kuathiri mimba!

Kutohudhuria kliniki na kutokufuata ushauri hasa wakati wa kujifungua kunaweza kuleta shida kubwa sana! Watoto wanaozaliwa wakiwa wamechoka wanahatari kubwa zaidi ya kuwa na uwezo mdogo wa kiakili au kupata shida za ukuaji na kudorora kwa hatua za kawaida za ukuaji! Haya yote uhathiri malezi ya mtoto!

Nani analea mtoto na kwa style ipi, hii nayo kesi nyingine
Changamoto hii ni kubwa mno kwa sasa!
Dunia ya leo mkizaa hakuna bibi, shangazi wala ndugu yeyote wa kuja kukusaidia kulea mwanao! Wengi huwa wanashughuli zao na hakuna mwenye muda wa kukusaidia mtoto! Kwa waajiriwa wanakuwa na amiezi 3 tu ya kulea mwanao kabla muajiri wako hajakutaka ofisini! Kimbembe kinakuwa pale zoezi zima la kulea baada ya miezi 3 linahamishiwa kwa housegirl! Kabinti kadogo ktk 12yrs - 18yrs anaachwa na kachanga, hakohako kafue, kampikie, kachote maji na shughuli Kibao na huku kama mshahara wa elfu 30 kwa mwezi ambazo kimekopwa!

Frustrations zinaanza na katoto kanaanza kuwa neglected mapema, baba anakuja usiku kulala na kudai posho ya kitanda tu, hachangii kabisa ktk malezi hasa kuhusu mahitaji ya kawaida ya mtoto! Hapa nazungumzia mtoto kubebwa, kubembelezwa, kuimbiwa nyimbo na kucheza naye! Wazazi huwa wanasema wanachoka kwa kuwa wametoka kuwatengezea "future" watoto wao, huku wakiwanyima the very "present"!!!

Tabia hizi za kuneglect watoto kidogo kidogo huota mizizi pale wanapoanza kutembea na kuwa busy na issues nyingine, Dada nao hutake advantages za kuwalisha viporo, au kuwatandika mirinda au Fanta hivyo vinakuwa vimevimbirwa na huwa havipigi kelele muda mwingi! Lkn kimsingi vinakosa mapenzi navyo kushindwa kujua jinsi yankupenda others!

Kuanzia mwaka wa 3, jukumu lote tunazibambikia shule na sisi tunaporomosha cash tu, dogo anatoka saa 12 alfajiri na anaingia saa 12 jioni eti yupo day care maana akikaa nyumbani anasumbua tu bora akae huko na wapo wanaohamishia watoto boarding tena hata nje ya nchi! Kiukweli hapa ndipo tunapowapoteza watoto kabisa! Watoto wanakuwa wageni nyumbani kwao, uhusiano wao na wazazi unajengwa kupitia taarifa za makarabrasha ya Mwl kuwa mtoto anafanya vizuri (muandiko au English au hisabati) as if quality ya mtoto hujengwa na ufaulu wa shule tu!

Tumeamua ku-compromise kila kitu ktk malezi na ukuaji wa watoto wetu just kwa ajili ya good grades tu za darasani! Mtoto hajengewi value nyingine zozote nje ya shule, so we are creating a robbot in the name of academia! Mtoto huyu sijui atakuwa mwana jamii wa aina gani? Sijui atarejesha kwa jamii, atawalinda na kuwapenda wazazi, ndugu, jamaa?? Hatothamini watu wengine, kwa kuwa huo msamiati hakuwahi kujengwa kichwani mwake, usishangae akiwa kiongozi akaiba kila kitu bila ya kuwa na huruma na jamii!

Labda ni summarise kwa kusema kuwa malezi ni changamoto kubwa ktk jamii ambayo kama ukitaka kuaddress changamoto hii, unapaswa kutazama maeneo mengi!
Tunaweza kujadili suala hili kwa upana zaidi, Ila nimeamua kuichokoza mada, najua wapo wabobezi watakaotusaidia kukuelewa somo kwa kina!
 
Day care day care day care,yamkini muasisi ni shetani ili kuharibu mpango sahihi wa malezi ya watoto na ndo mwanzo wa upendo kwa ndugu kupoa
 
Back
Top Bottom