Changamoto zinapojitokeza katika maisha yako elewa vitu hivi hapa

Changamoto zinapojitokeza katika maisha yako elewa vitu hivi hapa

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
427
Reaction score
575
Unapopitia changamoto katika maisha elewa mambo aya.

Katika dunia kila binadamu anapitia changamoto mbalimbali lakini uwezo wa kukabiliana changamoto ume tofautiana mtu na mtu kutokana na uzoefu wa maisha.

1.Changamoto zinakufanya kuwa imara, unapopitia changamoto katika maisha inabidi uelewe zipo changamoto zinazotokea katika maisha yako ni kwa ajili ya kukujenga kwa majukumu yako ya baadae, kuna wengine mmeandaliwa kuwa watu wakubwa na wenye ushawishi hivyo Mungu anawajenga ili kupata baraka alizo waandalia ili muweze kumiliki bila kuanguka,

Mfano kwenye bibilia ibrahimu, Musa, Daudi, Yusuph, bwana yesu kristo walipitia changamoto ngumu hii yote Mungu alikuwa ana wandaa kuwa wakuu .

2.Changamoto zinatokea kwa ajili ya kukuelimisha/kukufundisha, kuna changamoto zinatokea katika maisha yako ili kukusaidia kuweka mipaka, nidhamu ya fedha, muda, kukumbusha umuhimu wa kujipenda, kutambua thamani yako , kujua watu wako wa kweli, hivyo unapata elimu ya maisha kupitia changamoto ndio unakuwa mtu bora.

3.Changamoto zipo kusaidia kuibua uwezo wako au wazo kubwa, watu wengi waliofanya mambo makubwa idea wamezipata kwenye kipindi cha changamoto kama kukataliwa, kutengwa,N.k

Mfano Muanzilishi wa Alibaba, Jack Ma alipitia changamoto za kukataliwa kwenye kazi, maisha magumu, unapopitia changamoto ngumu ndipo Mungu anaweza kukupa idea kubwa na ni rahisi kuifanyia kazi maana akili yako inakuwa vizuri kipindi cha changamoto.

4.Changamoto zinatokea kutengeneza ushuhuda(testimony), muda mwengine Mungu ana ruhusu changamoto ili ujue nguvu yake katika maisha yako, kipindi cha changamoto ndio unaweza kutengeneza imani kwa Mungu,

Mfano kwenye Bibilia Mungu alikuwa anapeleka mapigo au changamoto misri kipindi mtawala pharoh ili wana waisrael wakiongozwa na Musa ili waelewe uwezo wa Mungu na kuwa na imani kwamba Mungu wanaye muabudu anauwezo , kuna wakati katika maisha yako kuna changamoto inatokea una sema bila Mungu hili nisingetoboa, Mungu anajenga imani yako au faith kipindi cha changamoto.
 
Sio kila jaribu linatoka kwa mungu...
Ila kulivuka jaribu lazima umuombe mungu
 
Back
Top Bottom