Deo Meck Mbagi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 360
- 525
Nitaandika kwa ufupi kwa sababu naangalia soka hapa.
Hapa nilipo naangalia mechi kati ya Zimbabwe na Senegal. Sote tunatambua kwa muda mrefu nchi ya Zimbabwe, kando ya changamoto za kisiasa za ndani, waliwekewa vikwazo na wamekuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi. Mazingira yake kwa namna yoyote sio mazuri ukilinganisha na Tanzania. Lakini je, inakuwaje nchi hii inaweza kuandaa timu yao vyema na kufudhu kucheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika? Je ni kwa sababu wana mapesa mengi kutuzidi au la?
Nimechukulia mfano mmoja wa soka, lakini katika michezo yote, ikiwemo hata ya kuogelea, japo tumezungukwa na water bodies nyingi bado hakuna mafanikio hata huko.
ukija riadha, tunao wamasai wanafukuza hadi swala kwa miguu ila bado hatuna wanariadha, what went wrong in Tanzania?
Ninashawishika kuamini kuwa tuna tatizo kubwa zaidi ya siasa ambalo linaturejesha nyuma, na bado kama jamii huenda hatujalitambua. Tunahitaji kufanya utafiti kuhusu tatizo tulilonalo kuliko kujifungia tu kwenye sababu za kisiasa, huku tukiacha za kijamii, kuna tatizo kubwa zaidi katika jamii yetu, naamini kuna jambo latakiwa kufanyiwa kazi katika hili.