Changamoto za soka la Tanzania

Bahimba

JF-Expert Member
May 8, 2013
510
346
Wadau natumai hamjambo na wazima wa afya, langu jioni hii ni dogo tu lakini ni kubwa sana kimtazamo, ni hivi karibuni pamejitokeza hali flani ya kishabiki ambayo si nzuri kwakweli katika mikakati ya kukuza soka letu.

Pamekua na hali ya kuitana majina ya hovyo kwa timu ambazo zinashindwa kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali, utasikia huyu ni kule, huyu nae utasikia anaitwa wa huku,,,,, jamani tunaelekea wapi??

Hivi karibuni katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Yanga alikua anachuana na timu moja toka Misri, lakini cha ajabu kabisa timu pinzani na Yanga ilidiriki kushangilia timu kutoka Misri na wakaenda mbali zaidi wakawa wanapeperusha mpaka bendera ya taifa ya Misri, nilishangaa sana.

Haya ni jana tu Yanga ilikua Misri katika mechi ya marudiano, na bahati mbaya Yanga ikatolewa, lakini pia jana niliendelea kushangazwa na mashabiki wa timu pinzani na Yanga kwa hapa Tanzania. Walilipuka kwa nderemo mara tu baada ya timu ya Misri kufunga goli lililopelekea kuitoa Yanga, jamani huu ndo ushabiki au wehu?

Tuliona wenzetu jana waarabu wote waliungana wakawa kitu kimoja sisi majuha, tunatengana nakubaki kuitana majina ya hovyo hovyo.

Rai yangu: Mashabiki wa soka Tanzania tuache ulimbukeni wa soka vinginevo hatutafika popote.
 
Ili haya yote yaishe viongozi wawe wa kwanza kubadilika unategemea kwa matusi ya Jely Muro kwa wanasimba waishangilie yanga? Never ever.
 
Watani wa jadi, huo ndo utani wenyewe. Kwenye makabila huja kutania kipindi cha msiba inakera ila ndo mila na desturi. Mbona hata simba ikicheza na timu za nje yanga huishaingilia timu za nje. Mm naanza kupata akili miaka ya 90 hii nimeikuta. Simba wanacheza na STELA abijan. Jamaa wakipata goli unasikia kelele km simba ndo imepata. Kipindi hicho tunasikiliza redio
 
Back
Top Bottom