Bei uliyosema 2320 ni selling rate ya benk, hyo 2250 ilikua ni buying rate ya benki. Hizi mwanzoni zilikua zinanichanganya.
Ukitaka zisikuchanganye kiurahisi fanya ni maongezi ya kuuziana kitu.
- - - - -
Scenario 1: USD ---> TZS
Mr Bank: Mr Mteja, karibu sana, nikuhudumie na nn?
Mr Mteja: Mr Bank, dah, nina dola za kimarekani hapa naziuza nipate tshs.
Mr Bank: Sawa sawa, hebu nizione...
Mr Bank: Sawa, sasa hizi nitanunua 2250 kwa kila dola 1, unasemaje? (buy rate)
Mr Mteja: Sawa haina shida... Nina dola kama 100 hapa.
Mr Bank: Sawa, haina neno.
(anakupatia 225,000 tshs).
- - - - -
Scenario 2: TZS ---> USD
Mr Bank: Karbu sana Mr Mteja, vp unahitaji nini?
Mr Mteja: Nina Tshs zangu hapa 225,000 nahitaj $ ya marekani aisee...
Mr Bank: Anhaaa, ninazo hizo nauza 1$ kwa 2320 tshs, unasemaje? (Sell rate)
Mr Mteja: Sawa nipatie.
(Unapokea $96.98)
- - - - -
Unapoenda na fedha ya kigeni mfano $ ukahitaji upate tshs, unaiuzia benki hyo pesa uliyokuwa nayo, kwahyo wao kama wafanya biashara watanunua kwa bei ndogo wakauze kwa bei kubwa baadae. Kwenye maongezi juu hapo, Hyo tofauti hapo ($3.02) ndo faida ya Bank, au Bureau.
Sent using
Jamii Forums mobile app