Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,705
Habari zetu wakereketwa wenzangu na wadau wa siasa kwa ujumla.
Naandika hili andiko katika hali ya kustaajabishwa kabisa na hali ilivyo sasa ndani ya chama cha mapinduzi katika hali ya ujumla ya kuibua damu mpya ya uongozi ndani ya chama.
Kwa wale wafatiliaji mtaungana nami kwamba approach wanazozitumia CCM katika kupitisha na pia katika kurithisha madaraka ni zilizopitwa na wakati kama si kuwa hazina maana wala mashiko.
Nimeshajaribu kutazama screening ya kupata viongozi wadogo ngazi ya UVCCM ambao wanatarajiwa kuja kuwa viongozi kwa tiketi ya chama hiki, nikagundua kuwa vigezo vinavyopewa kipaumbele ni vigezo dhaifu ambavyo hutengeneza ombwe la viongozi makini na kujaza majalibosi kama si viongozi vijana vilaza.
Zama za siasa za mazoea zimepitwa na wakati kwa maana tunaishi katika ulimwengu wa siasa mtambuka kwa hivi sasa. Jamii ya watanzania si tena ile ya kuletewa mfano wa viongozi ila ni jamii inayotaka vingozi mifano kwa maana ya kiongozi ambaye ana uhalali wa kisiasa both katika chama lakini muhimu zaidi katika taifa. Kiongozi mwenye politicall will na consciousness yaani kwa maana ya ufahamu.
Leo ukitazama vijana wengi wanaoshabikia kuingia katika nafasi za wazi za uongozi wa UVCCM na wanaojiandaa kuja kuingia katika tasinia ya uongozi kamili siku za baadae wengi wao ni waliojawa na mihemuko ya tamaa ya kuja kurithi nafasi za juu za uongozi ili kujipatia kipato kitakachowatoa katika umasikini huu uliokithiri kutokana na kukosekana kwa ajira especially kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu.
Kwa mara nyingi vigezo ambavyo hutumika katika kuwapa vijana maksi za kushika nafasi huwa mara nyingi ni purukushani alizofanya katika kukitangaza chama na kuimarisha mashina, hatua au level alizopitia hadi kufika alipofika kwa maana alishawahi kushika nyadhifa ngapi huko chini zinazohusiana na Chama cha mapinduzi. Hivi pamoja na vigezo vingine ambavyo siku vitaja huwa ndo CV ya kumpa max mtu katika kupata nafasi ya uongozi na hatimaye kwenda juu zaidi (rejea CV za Viongozi chipukizi)
Hili si jambo baya kwa maana ni vigezo ambavyo huonyesha commitment ya huyu kijana kwa chama. Ila sasa changamoto inakuja katika swala la uhalali wa kisiasa wa hawa wanaoitwa viongozi chipukizi waliopikwa kuja kushika nafasi za uongozi mbali mbali kwenye chama na taifa siku za usoni.
Nimekaa chini na kufanya utafiti wangu wa chini chini, wa kimya na wa umakini wa hali ya juu kwa kuwahoji hawa vijana maswali ya kinoko na kutazamia mrejesho wa majibu yao ( wengi hawakujua kuwa nilikuwa nipo katika utafiti). Ripoti yangu ikaniambia na kunionyesha kuwa hali si nzuri kwa kiwango kikubwa sana, na kama hawa na wengineo ambao sikuwahoji ndio wanatazamiwa kuja kushika kijiti ziku zijazo basi ni heri tu Chama cha mapinduzi kitafakari upya kuhusu kauli zake za tambo za kuamini kitakuwepo milele.
Haya ni baadhi tu ya majanga ambayo hata weww ukitafiti utayaona;
1.Vijana wengi wanaojiunga UVCCM na Uanachama kamili wa CCM kwa ujumla wao huko vyuo vikuu na uraiani wanatazama Chama hiki kama genge la kutafutia ulaji na si taasisi ya kisiasa ambayo inalengo la kushika mamlaka kwa lengo kuu la kuliletea taifa mendeleo yanayotakiwa na kututoa katika umasikini huu wa kujitakia.
2. Vijana na viongozi wanachama ndani ya UVCCM hujiona kama marole model wao badala ya wao kujiona kwa uhalisia na uwezo wao wa kuzaliwa nao na hii tayari inatosha kumnyima mtu sifa za kuwa kiongozi wa sasa na wa baadae katika nyanja yoyote ile. Ukitaka kudhihirisha hili naomba utazame namna Ndugu Pole pole, Makonda na viongozi chipukizi ndani wengineo (list ni kubwa) wa UVCCM namna wanavyoongea kwa kumuiga Baba wa taifa mwl. J.K nyerere, au kwa kumuiga Jakaya kikwete yaani ili waonekane kuwa ni perfect copy ya kiongozi anayemuiga.(Hili tatizo lipo hata CHADEMA NA CUF ambapo viongozi chipukizi huiga kila kitu na kuacha kuwa natural)
Tazama pia tabia na matendo kwa kuigana. Yaani vijana wanaamini katika kufanya shughuli za siasa kwa hila na mbinu za udanganyifu vitu ambavyo huwa wanafanya kwa kukopi na kupest kutoka kwa wale wanaowaita role models, wao huhisi kwa kufanya hivyo ni kuimarisha chama cha mapinduzi ila ukweli ni kinyume kabisa cha wanachodhania.
3. Vijana wa UVCCM sasa wameanzisha kajitabia ama wimbi la tabia za kujipendekeza na kujibananisha katika makwapa ya viongozi wakubwa wa CCM wakiamini hii ni mojawapo ya tiketi ama garantii ya kupenyezwa ama kupendekezwa katika kushika nafasi mbali mbali za uongozi katinga ngazi ya UVCCM na baadae ngazi ya Chama kitaifa. Si haba leo vijana kujitamba kuwa mimi ninapiga story na KINANA, NAPE NAUYE au utasikia mimi najuana na KIKWETE napiga naye story au utasikia Mzee Makamba kaniita ofisini kwake zote hizo zikiwa ni mbwembwe za kujidalali na kujinadi kwa wale wanaowatazamia. Hii ni Hasara kubwa sana kwa chama na taifa kama ndio tunataraji watu wa namna hii waje kushika nafasi za uongozi kitaifa.
4. Vijana wa UVCCM wameanza nao kama wazazi wao kujihusisha na siasa za makundi ambazo huwa zinalenga kutengeneza wafuasi wa kiongozi mojawapo katika ngazi za kitaifa. Katika hili, vijana hujikuta wakiwa ni vibaraka wa kutimiza maelekezo ya kiongozi fulani na kiasahau ajenda ya kujenga chama ila jitihada huelekezwa katika kufanyiana fitina majungu na hila za kipumbavu ambazo hazina tija yoyote. Ukilihoji hili Viongozi walezi wa chama watakuhakikishia kuwa halipo ila niamini lipo na linakuwa kwa kasi tena zaidi nyakati za chaguzi kuuu.
5. Narejea tena hoja ya uhalali wa kiasiasa na kutanabaisha kuwa wimbi la vijana wapya wanaochipukia katika ulimwengu wa siasa ( na hili lipo vyama vyote vya siasa hususani hivi vikubwa vitatu) hawapo political conscious kwa maana ya kujua nyakati zimebadilika na hivyo basi hata changaoto za jamii ya watz zinabadilika kila uchao ila wao bado wanaamini kuwa tz bado ni ya mwaka 47 na hivyo basi wanaendeleza tamaduni zile zile ili kuwafurasha role models wao na kusahau kuwa wao ni kizazi kipya na hivyo basi wanatakiwa kuqa chachu ya mabadiliko kwa kuadopt mbinu na mitazamo mipya ya kisiasa yenye tija kwa taifa na chama chao badala ya kuwa puppets wa kupokea na kuendeleza mifumo ya kizamani ambayo inawafanya kuwa predictable mbele ya watz na vyama vya upinzani kama chadema na vile basi wanakosa mbinu mbadala za kukisafiaha Chama Cha mapinduzi kwenye jamii badala yake wanaendeleza msururu wa matukio na vitendo ambavyo havina uhalali kisiasa na wamebebelea hoja hafifu vichwani mwao kitendo ambacho kinazidi shusha thamani ya CCM kila uchao katika jamii na kukibakisha kuwa ni chama cha wapigaji na wapenda hila. Madhara ya kutokuwa political conscious inajenga vijana ambao wanapopewa nafasi za uongozi wanafeli ku deliver mabadiliko na kuwa msaada kwa taifa. Mifano hai inaonekana wazi tazama akina Makonda , polepole wanavyopata shida kuendesha ofisi za mkoa na wilaya kwa kufanya mambo ambayo yanaharibu sifa ya chama na wanafanya tu ili kupata publicity ila hukuna tija kwa taifa katika taifa. Nape Nauye anaendeleza uozo ule ule wa wazee waliopita katika wizara tuliamini pengine kwasababu ni kijana ataleta utofauti ila ndio hivyo tena ukipanda chungwa usitarajie kuvuna apple.
Nina mengi sana ya kusema ila wino wa sim umeniishia nitaendelea nikiongeza. Lakini katika kuhitimisha, napenda kutoa ilani kwa chama cha mapinduzi. Wazee na walezi wa vijana ndani ya chama. Hebu mjitafakari juu ya ajenda yenu ya kuingiza damu mpya katika chama. Ni wazi na ni kweli CCM imezembea sana kipindi cha katikati hapo kwa kufanya madudu ya kila aina. Aibu ya hayo madudu tumeibeba watanzania sote bila kujali chama. MUNGU ameweza kuwakingia kifua kwa mida wa miaka yote hii 50+ ya umri wa mtu mzima, ameweka mkono kifuani kwa kila mtanzania akimtaka awe na uvumilivu na subira jambo ambalo chama cha mapinduzi na wadau wake wanahisi ni jitihada zao na kuhisi wapo sahihi bila dosari.
Leo hii , pamoja na kushuka idadi vijana mahiri ( ukimtoa HUSSENI BASHE pale bungeni na hayati filikunjombe) wa kupeperusha bendera ya chama imefikia hatua inapokea tu usajiri wa wanachama wapya hovyo wakiwamo Mashangingi, mateja, wahuni, akina mama mashakumpe ambao kazi yao ni kusubiria kampeni ili washangilie kwa kelele zisizo na mbele wala nyuma, kupiga tambo za kijinga na kucheza taarabu na kidumange utadhani hicho ni chama cha mashangingi kitu ambacho ni aibu kwa chama chenye hadhi na historia nzito sana kimataifa. Leo hii aibu inatuadhirisha sote kama taifa bila kujali kama ni wanachama au la.
Fikeni wakati mjitathimini,MUNGU amechoka kuwakingia kifua kwa watanzania maana sasa hata yeye anajua amewapa mamlaka msiyo stahili na mnacheza na kitu nyeti sana kinachoitwa serikali. Rejeeni nguzo za chama.....tafuteni vijana kwa utashi wa matendo yao ya asili na si vijana wasanii ambao watnatumia Chama kama genge la kujitafutia kipato badala ya kujenga nchi. Fanyeni screening binafsi ya kuwachambua vijana kwa uwezo na utashi wao halisi na si kwakujifunza kwa kupita pita vinyazifa vya kipuuzi kama sijui mwenye kiti wa UVCCM taifa mara sijui katibu wa shina. Haya mavigezo ya kipuuzi ndio yanawafanya mnapata wabunge na watendaji zero ambao hata bungeni wanashindwa kumuwekea mh. rais kinga dhidi ya mashambulizi ya malalmiko ya wapinzani kwa kuongea pumba wanabaki kuwaachia wabunge wachache kama Mh. Hussein Bashe ambaye ndio at least huwa anaokoa jahazi kwa kuongea mambo ya msingi na kupangilia hoja kwa mantiki ( utasikia mbunge kilaza anaropoka tu hovyo "HATA MSEME NINI CCM NI MBELE KWA MBELE"). Hii inawafanya kuwa na wanachama duni machoni kwa watanzania.
Shughulikieni hii kitu kama sivyo mnajichimbia kaburi taaratibu Mh. Raisi Magufuri atakapomaliza muda wake.
Ni hayo tu ntarejea baadae.